Na Jusline Marco-Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Ndg.Jerry Muro amefanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa miundombinu wa vyumba vya madarasa pamoja na vyoo katika shule za msingi wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari Muro alisema kuwa kupitia kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya yake kwaajili ya shule za sekondari waliweza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa asilimia zaidi ya 90 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo kwa mwaka huu.

"Zoezi hili tumelielekeza maalumu kwenye shule za msingi na kupitia kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa tumepokea watoto wote ambao wanapaswa kupokewa katika shule zetu za sekondari".Alisema Muro

Aidha alieleza kuwa katika zoezi la upokeaji wa wanafunzi hao kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wanafunzi kutoripoti katika shule walizochaguliwa kutokana na wazazi wao kuwa miongoni mwa jamii ya kuhamahama kutafuta malisho ya mifugo yao.

"Tulichunguza kwanini watoto hao hawajaripoti shuleni,tukagundua wazazi wao ni jamii ya wafugaji ambao wanahama na mifugo kutafuta malisho ambapo tulibaini kuwa wamehamia katika upande wa Longido."Alieleza Muro

Aliongeza kuwa zoezi hilo la ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari wilayani humo limemalizia ambapo sasa hivi wapo katika zoezi la ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi wilayani humo.

Vilevile Muro alitolea ufafanuzi wa picha ya choo cha shule ya Olimringaringa ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii hasa mtandao wa jamii forum siyo picha halisi ya choo cha shule hilo ambapo alisema kuwa wanatambua changamoto ya matundu ya choo hayatoshi kulingana na idadi ya wanafunzi ambao hupokelewa kwenye shule za msingi na katika maeneo mengine.

"Hakuna shule kwenye wilaya ya Arumeru yenye choo kama kile,Shule ya Olimringaringa ina choo chenye matundu 18 kwa 16 hivyo katika awamu hii tunachofanya kwenye wilaya ya Arumeru ni ujenzi wa vyoo na madarasa mengine kwenye shule za msingi.Alisema Muro

Vilevile aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi 9,kampeni inayoendelea niya ujenzi wa vyumba vya madarasa 50 na matundu ya vyoo 120 ambapo kuanzia mwezi huu wa 4 hadi mwezi wa 12 mwishoni ujenzi huo utakuwa umekamilika ambapo ujenzi huo umeanza katika shule za Olimringaringa,Olosiva,Mringa,Oldonyowasi ambapo aliweza kufanya ziara ya kuhimiza kamati za shule kwa kushirikiana na wazazi kuweza kujenga madarasa na matundu hayo ya vyoo.

Sambamba na hayo DC Muro alieleza kuwa katika Wilaya yake kuna zoezi endelevu ambalo limefanyika takribani wiki mbili la kuthibiti na kukamata mtandao wa wezi wa mifugo ikiwemo ng'ombe na mbuzi.

"Tulifanya zoezi hili hasa kwenye kipindi cha sherehe za Pasaka tukiwa tunalenga kuhakikisha katika kipindi cha sherehe ya sikukuu ya Pasaka kunakuwa hakuna mwananchi anayekumbwa na adha ya wizi wa ng'ombe,mbuzi,kuku au bata."Alisema Muro

"Imezoeleka katika baadhi ya maeneo nyakati hizi za majira ya sikukuu ndiyo nyakati ambazo watu wanaendesha mtandao wa wizi wa mifugo ya watu."Aliongeza Mkuu huyo wa Wilaya

Alieleza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja kumekuwa na wizi wa ng'ombe takribani 31 katika maeneo kadhaa huku maeneo sugu yaliyokithiri kwa wizi huo yakiwa ni maeneo ya Kata ya Kikwe,Akheri pamoja na Mulala ambapo baada ya kupokea taarifa za wizi huo walihakikisha wanaendesha operesheni kwa kushirikiana na wananchi kutafuta taarifa zitakazo wasaidia kuwakamata wezi hao na wahusika.

Aliongeza kuwa operesheni nyingine amabayo inaendelea ni utekelezaji wa mtandao huo wa wizi wa ng'ombe ambapo wamefanikiwa katika Tarafa ya Mukulat,Ngaramtoni,Oldonyowasi,Oldonyosambu na walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 9 ambao baadhi walikiri kuiba mbuzi na ng'ombe na kuwakabidhi katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.

Kutokanana uchinjaji holela unaofanywa na wezi wa mifugo hiyo ipo sheria ya mazingira inayoelekeza kuwepo kwa  maeneo maalum kwa ajili ya machinjio ambayo kimsingi ndiyo yanayotakiwa kufanyika shughuli za uchinjaji huku sheria ya utunzaji mazingira ikielekeza uchafu unaotokana na shughuli za uchinjaji uwe wa namna gani.

Pamoja na hayo aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa zitakazo wasaidia kuwaibua wezi hao ili kuweza kudhibiti na kutokomeza mtandao huo.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha Ndg.Jery Muro akizungumza na wananchi katika Opareshi ya kukamata na kudhibiti mtandao wa wezi hao wa mifugo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...