Taasisi ya Flaviana Matata Foundation chini ya Mwanamitindo Flaviana Matata imetoa taulo za kike (Sanitary Pads) kwa Wasichana wenye uhitaji 100 kutoka Shule ya Wasichana ya Jangwani, huu ni mwanzo wa kugawa taulo hizi kwa Wasichana watakaonufaika na Kampeni yao ya 'Donate A Period'. kupitia vituo vya mafuta vya TOTAL.

“Wasichana hawa watapata taulo za kike bure kwa mwaka mzima ambapo kila Msichana atapata “packet” moja na nusu kila mwezi, kipekee kabisa tunawashukuru TOTAL na kila aliyeshiriki kwa kujitoa kwao kuhakikisha tunawafikia Wasichana wengi zaidi kwa kujaza mafuta katika vituo vya TOTAL kwa mwezi March”,alisema Flavina

Alisema kuwa jumla wamepokea kiasi cha Tsh. 18,184,003 ambazo zinasaidia Wasichana 420 kwa mwaka mzima, kila Msichana atapokea paketi 18 kwa mwaka, hivyo inafanya idadi ya Wasichana wanaopokea taulo zetu bure kila mwezi kufikia 1720 kwa ujumla na kati ya hao 300 ni kutokana na asilimia 10 ya faida inayopatikana katika mauzo ya Lavy Sanitary pads. 

“Tunatambua hedhi ni kikwazo kwa wasichana wengi wanao toka kwenye mazingira magumu kote mijini na vijijini kukosa masomo siku 3-5 kila mwezi kwa sababu hawawezi kumudu gharama za taulo za kike, tutawahiza Wadau mbalimbali kuunga jitihada hizi kwa namna moja au nyingine tuhakikishe hedhi siyo kikwazo kwa Mtoto wa Kike kupata elimu”,alieleza Flavi
na.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...