Na Woinde Shizza, ARUSHA.


MAHAKAMA , kuu masijala Ndogo ya kazi Kanda ya Arusha leo imeahirisha kesi ya madai dhidi ya kampuni ya Tan communication inayomiliki kituo cha  Radio Five baada ya upande wa wadaiwa kutokuhudhuria mahakamani na kushindwa kutoa taarifa.

Hakimu mkazi , Nguvava,ameahirisha kesi hiyo ambayo ilikuwa kwa ajili ya kusikiliza pingamizi lililowekwa na upande wa wadaiwa  hadi Juni 11 mwaka huu.

Wafanyakazi Saba wa radio hiyo wakiongozwa na Jofrey Steveni,walifungua kesi namb 151 ya mwaka 2020, wakikidai kituo hicho cha utangazaji cha radio five zaidi ya sh, milioni 31.9 baada ya kuachishwa kazi kinyume na utaratibu.

Wafanyakazi hao walifungua kesi mahakamani hapo baada kutoridhika na uamuzi uliotolewa na mahakama ya usuluhishi (CMA) baada ya kumpa ushindi mdaiwa.

Upande wa walalamikaji wanaongozwa na wakili Heri Makando waliiomba mahakama hiyo itoe idhini ya kukamatwa Mali za mdaiwa ambaye ni Tan Communication na kupigwa mnada ili kufidia malipo ya wafanyakazi hao.

Wafanyakazi hao waliimba mahakama hiyo itoe amri ya kukamatwa kwa Mali za madaiwa,ambazo ni pamoja na Jengo la kituo hicho cha utangazaji cha Radio five,lililopo Njiro plot namb 153 n.a. 154 block J,Genereta ,vifaa vya studio pamoja na vifaa vya kufusyia  matangazo.

Upande wa mdaiwa,ambao uliwakilishwa na wakili ,Andrew Maganga aliwasilisha notisi mahakama kuu ya rufaa kusudio la kupinga hukumu iliyotolewa na jaji Johannes Masara , June 16 ,2020 iliyowapa ushindi wadai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...