Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde, akifungua Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli, akizungumza wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayesimamia Elimu ya Awali na Msingi ambaye pia ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Suzan Nussu, akizungumza wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Moses Chitama akichangia mada katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi, Maadili na Nidhamu kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Mwalimu Robert Likwolela akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Tume wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi, Ajira na Maendeleo ya Walimu kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), akichangia mada wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Maafisa Elimu Kata, Wilaya ya Kyerwa, Oscar Tumwesige, akichangia mada wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Maafisa Elimu Kata, Wilaya ya Bagamoyo, Hamisi  Mwanankuta, akichangia mada wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Maafisa Elimu Kata, Wilaya ya Muheza, Danstan Mahiza, akichangia mada wakati wa siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde (katikati) akiungana na Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, kuimba Wimbo wa Taifa, muda mfupi kabla ya kufungua Mkutano huo Aprili 8, 2021 jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu, TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Moses Chitama (kulia-mbele) na Mkurugenzi Msaidizi, Ajira na Maendeleo ya Walimu Mectildis Kapinga (wa tatu kutoka kushoto – mbele), wakiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, wakifuatilia mkutano huo katika siku ya kwanza, Aprili 8, 2021 jijini Dodoma.

******************************

Na Veronica Simba – TSC

Maafisa Elimu Kata kote nchini wametakiwa kutimiza wajibu wao wa kutoa msaada wa kitaaluma ili kuwawezesha walimu katika maeneo yao kufundisha kwa ufanisi na hivyo kuboresha kiwango cha elimu.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde, alipokuwa akifungua Mkutano wa Viongozi wa Maafisa Elimu Kata, Aprili 8 mwaka huu, jijini Dodoma.

Aidha, Naibu Waziri Silinde, amewataka Maafisa Elimu Kata kusimamia kikamilifu ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari huku akieleza kuwa imebainika baadhi ya Maafisa hao hawasimamii shule za sekondari.

“Mnajikita zaidi katika shule za msingi na kujisahau kusimamia shule za sekondari. Kote ni wajibu wenu na hakuna mtu anayepaswa kuwazuia. Akijitokeza wa kuwazuia tupeni taarifa tutamchukulia hatua,” alisisitiza.

Akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Tume ya Utumishi wa Walimu katika Mkutano huo, Mkurugenzi Msaidizi, Maadili na Nidhamu, Mwalimu Robert Likwolela aliwataka Maafisa Elimu hao kushughulikia makosa yanayofanywa na walimu, ambayo hayapewi umuhimu kwa kudhaniwa ni madogo.

Akifafanua, Mwl. Lwikolela alitoa mfano wa kosa la utoro kwa walimu kuwa pamoja na kuathiri utoaji elimu lakini limekuwa halitiliwi maanani kwa kuchukuliwa kama halina uzito.

“Wako baadhi ya Walimu hata hawaandai Mpango wa Somo (Lesson Plan) na wanafundisha vipindi vichache tofauti na walivyopangiwa lakini wanaachwa tu. Ni wajibu wenu kuwafuatilia hao na kushirikiana na Wakuu wa Shule katika kuwarudisha kwenye mstari.”

Hata hivyo, akitoa ufafanuzi zaidi katika masuala ya nidhamu kwa walimu, Mkurugenzi Msaidizi, Ajira na Maendeleo ya Walimu, Mectildis Kapinga, alisema endapo Mwalimu atabainika kutenda kosa, anayepaswa kutoa adhabu kwake kwa mujibu wa sheria ni Mamlaka yake ya Nidhamu ambayo ni Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), na siyo vinginevyo.

Hivyo aliwatahadharisha Maafisa Elimu Kata kutojichukulia sheria mkononi badala yake, ikitokea wamebaini Mwalimu anakiuka maadili ya kazi yake, washirikiane na Mkuu wa Shule kumkanya ili abadili mwenendo wake na asipojirekebisha wamripoti kwa Mamlaka yake ya Nidhamu ili imchukulie hatua.

Kwa upande wake, akitilia mkazo suala la uwajibishaji walimu wanaokiuka maadili ya kazi, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kutoka TSC, Moses Chitama, alishauri kabla ya muhusika kuripotiwa kwa Tume, zifanyike jitihada katika ngazi ya shule na kata, kukaa na kuzungumza naye ili kumkanya, hususan kwa makosa madogomadogo ambayo yanarekebishika.

Mkutano huo wa Maafisa Elimu Kata unatarajiwa kuhitimishwa rasmi Aprili 9, 2021 ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...