Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika akiuliza swali kwa Serikali kwamba inachukua hatua gani kumaliza tatizo la upungufu wa Walimu nchini hasa shule zilizopo maeneo ya vijijini. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA


Na Richard Mwaikenda, Dodoma

Dodoma.Spika, ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa walimu katika Shule za Msingi na Sekondari, Serikali imeahidi kuendelea kuajiri walimu ili kuziba pengo hilo. Kauli hiyo ilitolewa bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi David Silinde wakati akijibu swali la mbunge wa Njombe mjini Deodatus Mwanyika (CCM). 

Naibu Waziri amesema kuanzia Disemba 2015 hadi Septemba 2020, Serikali imeshaajiri walimu 10,666 wa Shule za Msingi na Walimu 7,515 wa Shule za Sekondari na ambapo wamepangwa kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa. Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua Serikali inachukua hatua gani kumaliza tatizo la upungufu wa Walimu nchini hasa shule zilizopo maeneo ya vijijini. 

Katika swali la nyongeza Mwanyika ameuliza iwapo Serikali itakuwa na mkakati thabiti wa kuajiri walimu wengi kutokana na utoaji wa elimu bure ulioongeza idadi ya wanafunzi na kuangalia maeneo yenye uhitaji mkubwa. Silinde alisema, katika kipindi cha Desemba 2015 hadi Septemba 2020, Halmashauri ya Mji Njombe imeajiri walimu 21 wa Shule za Msingi na 111 wa Shule za Sekondari. 

"Vilevile Ofisi ya Rais-Tamisemi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itaajiri Walimu wapya 6,000 wa Shule za Msingi na Sekondari ifikapo Juni 2021 ili kujaza nafasi zilizoachwa na Walimu waliofariki ama kustaafu kazi," alisema Silinde. 

Alisema Tamisemi imekuwa ikifanya uhamisho wa ndani kwa kuwahamisha walimu waliozi katika maeneo ya mijini na kuwapanga kwenye Shule zenye uhaba wa walimu ambazo nyingi zipo maeneo ya vijijini. 

Kwa mujibu wa Silinde, Serikali itaendelea kuajiri na kuwapanga walimu kwenye Shule za Msingi na Sekondari hasa zenye mahitaji makubwa kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video Mbunge Mwanyika akiibana Serikali kuhusu suala hilo na Naibu Waziri wa Tamisemi, Silnde akijibu....

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
 0754264203

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...