Naibu Kamishana wa NCAA anayesimamia Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii Dkt. Christopher Timbuka (kulia) akipata maelezo kutoka kwa watalaam wa uzalishaji wa Mizinga ya Nyuki kutoka karakana ya Center Park Bees iliyoko mkoani Dodoma.Mtaalaam wa Nyuki kutoka kiwanda cha Nyuki cha TFS Manyoni akiwaonyesha Wajumbe wa NCAA mashine ya kisasa inayotumika kuchakata mazao ya Nyuki katika kiwanda hicho.

Muonekano wa asali bora iliyofungashwa kutoka kiwanda cha uchakataji mazao ya asali kinachomilikiwa na  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kilichpo Manyoni Mkoani Singida.

Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya NCAA wakipata elimu kuhusu uchakataji wa mazao ya asali kutoka kwa msimamizi wa kiwanda ya Nyuki TFS Manyoni Bw. Ramia Konyo.

**************************

Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wamefanya ziara ya mafunzo ya siku mbili katika viwanda vya uzalishaji, na uchakataji wa mazao ya Nyuki vinavyoendeshwa na kusimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Manyoni na kingine cha CPB (Central Park Bees) kilichopo Jijini Dodoma.

Akizungumza katika ziara hiyo Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii wa NCAA Dkt. Christopher Timbuka ameeleza kuwa ziara hiyo imelenga kupata ujuzi wa uanzishwaji, uendeshaji na usimamizi wa viwanda vya mazao ya Nyuki kwa watalaam wa TFS na CPB ili NCAA itumie utaalam huo kujenga kiwanda kwa ajili ya kuchakata na kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ya nyuki kwa wananchi wa kata 11 zilizopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro na maeneo jirani na Hifadhi hiyo katika Wilaya za Karatu, Meatu na Monduli. 

“ NCAA tuna jukumu la kuendeleza Jamii inayoishi ndani ya Hifadhi, tayari tumeanzisha miradi ya ufugaji nyuki kwa kata 11 zilizoko ndani ya eneo na tuna mpango wa kujenga kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki nje ya eneo la Hifadhi ili kuongeza thamani ya asali inayozalishwa ndio maana tumekuja kwa wenzetu wa TFS na CPB kuona namna walivyofanikiwa katika utekelezaji wa miradi ya ufugaji nyuki” alisema Dkt. Timbuka.

Dkt. Timbuka ameongeza kuwa pamoja na kutembelea viwanda hivyo, ziara hiyo pia imelenga kutembelea kiwanda cha Centre Park Bees kufuatilia maendeleo ya utengenezaji wa mizinga ambayo NCAA imeinunua kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ufugaji nyuki kwa wananchi ili kuwaongezea mnyororo wa thamani ya mazao ya nyuki    (beekiping value chain Management).

Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimania idara Maendeleo ya Jamii Bw. Fedes Mdalla amebainisha kuwa tayari NCAA katika mwaka ujao wa fedha imepanga kujenga kiwanda cha kuchakata mazao ya Nyuki ili kuviwezesha  vikundi vya ufugaji nyuki 25 vinavyozalisha mazao ya nyuki kuzalisha kwa uhakika na kufungasha asali katika namna bora inayokidhi mahitaji ya soko. 

Kwa upande wake Kaimu Msimamizi wa Kiwanda cha kuchakata mazao ya Nyuki kutoka TFS Bw Ramia Athumani Konyo ameeleza kuwa katika msitu wa Kirimu wenye ukubwa wa hekta 15,652 wameweka jumla ya mizinga 5000 inayosimamiwa na vikundi vya nyuki 10 ambavyo viko kwenye Halmashauri za Manyoni na Itigi Mkoani Singida. 

“Mwaka 2019 tulipoanzisha kiwanda hapa Manyoni TFS kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumeshatoa elimu ya namna ya kufuga, kutunza mizinga na nyuki, kurina asali, kufungasha na kutafuta masoko na baada ya elimu tuligawa mizinga 500 kwa kila kikundi, tangu tulipoanza utaratibu huu tumeshapata mafanikio makubwa yaliyoiwezesha TFS kuzalisha wastani wa tani 3-6 kwa kila mwaka.

Bw. Konyo ameongeza kuwa mpango wa NCAA kuanzisha kiwanda cha Uchakataji wa mazao ya Nyuki Wilayani karatu si tu kwamba kitasaidia wafugaji Nyuki wa Ngorongoro ndani bali pia utasaidia kukidhi mahitaji makubwa ya asali kwa soko la ndani na nje ya Nchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...