MFANYABIASHARA, John Kyenkungu 65, anayeishi Eneo Mikocheni Mkoani Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kughushi hati ya nyumba ili kuchukulia mkopo.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali, Adolph Lema amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando kuwa katika tarehe isiyojulikana mwaka 2014, mshtakiwa Kyenkungu alitenda kosa la kughushi hati hiyo.

Imedaiwa, siku hiyo mshtakiwa kwa nia ya kudanganya alighushi hati ya mkopo ya mwaka 2014 na kusaini kwamba Said Nassoro amekubali kutumia hati ya nyumba yake yenye namba 25480 kiwanja namba 516 kitalu B, iliyopo Mikocheni kama dhamana ya kupata mkopo kutoka benki ya Equity huku akijua kuwa siyo kweli.

Imeendelea kudaiwa kuwa, Agosti 23, 2014 jijiji Dar es Salaam mshtakiwa alighushi barua ya 23/8/2014 kwamba Said Nassoro amekubali kutumia hati ya nyumba yake yenye namba 25480 kiwanja namba 516 kitalu B, iliyopo Mikocheni kama dhamana ya kupata mkopo kutoka benki ya Equity huku akijua kuwa siyo kweli.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamama yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya Sh. Milioni 100 kila mmoja huku mshtakiwa akitakiwa kuweka fedha taslimu sh. Milioni 75 au hati ya mali isiyohamishika ya kiasi hicho cha pesa.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi Aprili 21, 2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...