Serikali imetenga shilingi milioni 311.9 zitakazotumika kuchonga Barabara yenye urefu wa kilometa 20 katika hifadhi ya Taifa Rumanyika karagwe na kilometa 51 katika Hifadhi ya Taifa ya Ibanda Kyerwa katika mwaka wa fedha 2020/2021.
Kauli hiyo imetolewa leo
Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary
Masanja wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Kyerwa Mhe. Innocent
Sebba Bilakwate (CCM) ambaye alihoji kuhusu mpango wa Serikali wa
kuweka miundombinu mizuri ya Barabara katika hifadhi hizo Ili kuvutia
watalii.
Akijibu Swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na
Utalii Dkt Damas Ndumbaro ,Mhe. Masanja ameeleza kuwa hifadhi za Taifa
za Ibanda Kyerwa na Rumanyika karagwe zilianzishwa kupitia tangazo la
Serikali Na 509 na 510 la tarehe 5/7/2019 .
Amesema hifadhi hizo zilitokana na kupandishwa hadhi kwa yaliyokuwa mapori ya akiba ya Ibanda na Rumanyika .
"Ili
kuwezesha hifadhi hifadhi hizo kufikika kwa urahisi Serikali kupitia
TANROADS na TARURA iliyokuwa ikitengeneza Barabara mbalimbali
zinazorahisha kufika kwa watalii katika hifadhi hizo , Barabara hizo ni
pamoja Mgamkorongo iliyopo wilaya ya korogwe hadi murongo wilayani
Kyerwa yenye urefu wa kilometa 112 ambayo inafanyiwa matengenezo na
TANROADS kila mwaka na imewekwa katika mpango wa Kujengwa kwa kiwango
cha lami katika mwaka wa fedha 2020/2021" Amesisitiza Mhe.Mary Masanja.
Aidha,
amesema jitihada hizo za kuboresha miundombinu ya Barabara katika
hifadhi ya Taifa Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe na maeneo mengine
yote ya hifadhi zitasaidia kuweka Mazingira mazuri yatakayowezesha
hifadhi hizo kutembelewa na watalii wengi wa maeneo ya karibu pamoja na
wageni kutoka nchi jirani.
Kuhusu ulinzi wa maeneo hayo ameeleza kuwa wizara imekuwa ikiyaanisha maeneo yote na kuweka mipaka.
"
Katika hifadhi ya Ibanda Kyerwa na Rumanyika tulifanya tathmini baada
ya wataalamu wetu kuainisha mipaka, utekelezaji wake tunaendelea nao
kwa kuandaa Mazingira ya kuwapeleka wataalamu kwa ajili ya gharama za
uthamini na kuanisha maeneo ambayo yanachangamoto za uhifadhi "
Amesisitiza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja akiwasili
katika viwanja vya Bunge kuhudhuria mkutano wa 3 wa Kikao cha 5 cha
Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mapema leo April 08, 2021
Jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...