Kampuni ya kimataifa ya Millcom International S.A ambayo ni kampuni mama ya kampuni za simu za Tigo Tanzania na Zantel inatangaza kuwa imeingia katika makubaliano na Axian Group, kampuni ya kimataifa iliyoko Antananarivo-Madagascar ili kuiuzia umiliki wa kampuni hizo mbili zilizopo Tanzania.

Hatua ya kuziuza kampuni hizo kwa Axian Group ni sehemu ya mkakati wa Millicom kujikita katika utoaji wa huduma za simu katika ukanda America ya Kusini (Latin America) baada ya kufanya uwekezaji mkubwa katika kuendeleza sekta ya mawasiliano barani Afrika kwa takribani miaka 25.

Ujio wa kampuni ya Axian Group kwenye soko la Tanzania utawezesha kuongeza wataalamu katika sekta ya mawasiliano ambao wamefanikiwa kutengeneza na kukuza nembo na biashara nyingi katika ukanda wa bahari ya Hindi, Afrika pamoja na Ulaya.
Axian Telecom ni moja ya kampuni tanzu inayoongoza kutoa huduma za mawasiliano nchini Madagascar, Visiwa vya Reunion, Mayotte na Comoro pamoja nan chi za Senegal na Togo.

Millicom inafarijika kumpata muwekezaji mahiri kama Axian ambaye amejizatiti katika kuendeleza mipango ya muda mrefu iliyowekwa na Tigo na Zantel ili kuhakikisha zinatoa huduma nafuu, za uhakika na za kibunifu kwa watanzania.

Katika kutekeleza hayo, Axian imepanga kufanya yafuatayo:
• Kufanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ili kuongeza ushindani, kuboresha uendeshaji pamoja na kuhakikisha mageuzi ya uchumi wa kidigitali.
• Kupanua wigo wa huduma za mawasiliano na kuchochea mageuzi ya kidigitali katika nchi ya Tanzania.
• Kuchochea ujumuishwaji wa watu kiuchumi ‘Financial Inclusion’ pamoja na kuongeza ubunifu kwenye huduma za fedha
• Kuhimiza ukuaji wa taaluma kwa wafanyakazi kupitia mafunzo ili kufanikisha malengo yaliyowekwa.

Tunapenda kuwahakikishia wadau na umma kwa ujumla kuwa, uendeshaji wa biashara utabaki kama ulivyo hadi pale tutakapopata vibali na uthibitisho kutoka kwa mamlaka husika.Pia tutaendelea kuwapa wateja wetu huduma bidhaa na huduma bora.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1995, Kampuni ya Millicom Tanzania (Tigo) kupitia azma yake ya kuleta mageuzi ya kidigitali, ilikuwa ya kwanza kuzindua GSM na mtandao wa 3G nchini Tanzania.

Mnamo Aprili 2014, Tigo ilizindua mtandao wa 4G katika jiji la Dar es Salaam na ilipofika mwaka 2016, mtandao wa 4G ulikuwa umeenea katika mikoa yote ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...