Zainab Nyamka, Michuzi Tv

WANANCHI wa Wilaya ya Mkuranga waanza kunufaika na mradi wa Mkubwa wa Maji uliotumia takribani Bilion 5.6 hadi kukamilika.

Mradi wa Maji Mkuranga umetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ili kuondoa adha ya maji ya muda mrefu kwa  wakazi wa eneo hilo.

Mamlaka imewezea kutumia fedha za ndani kukamilisha mradi huo ambapo zoezi lililobaki ni kuanza maunganisho mapya kwa wateja walioomba kupatiwa huduma ya maji safi.

Akizungumzia kukamilika kwa mradi huo, Mhandisi wa DAWASA Mkuranga Richard Katwiga amesema tayari maji yameshaingia kuanzia Aprili 02, mwaka huu katika tanki lenye ujazo wa lita 1.5 na leo mafundi watafungulia ili kuweza kuyaruhusu maji kusafisha mtandao wa mabomba waliyoyalaza kabla ya kuanza kupeleka huduma kwa wateja.

Amesema, wamelaza mtandao wa mabomba takribani km 65 katika kata ya Mkuranga na Kiparang'anda ambazo zitaanza kufaidika na mradi huo kwenys awamu ya kwanza kabla ya kwenda maeneo mengine ya karibu.

"Maji tayari yameshaingia katika tanki letu hatua iliyobaki ni kuyaruhusu kutoka ili yakasafishe mtandao wa mabomba ambao tumeulaza kwa km 65 kwenye kata za Mkuranga na Kiparang'anda," amesema.

Katwiga amesema, wapo wananchi walioathirika wakati wa ujenzi wa mradi wa Mkuranga lakini kufikia Oktoba 2019 walianza kupata huduma ya maji kupitia mtandao mpya wa mabomba waliyoyalaza kwa kutumia tanki la zamani lililojenga mwaka 2002

Aidha, amesema kuanzia Aprili 9 mwaka huu wanatarajia kufanya maunganisho ya tanki kubwa la maji kwenye mtandoa mpya ili wananchi waendelee kupata huduma kama kawaida na kuanza kufanya maunganisho mapya kwa wateja waliofanya maombi.

"Kuna jumla ya wateja 50 wameshaomba kuunganishiwa huduma ya maji, tutaanza kuwatembelea ili kuwaunganishia huduma ya maji na zaidi lengo la Dawasa ni kuwafikia wananchi wengi zaidi ndani ya mji wa Mkuranga," amesema Katwiga

"Lengo letu ni kukusanya milion 60 kwa mwezi na hilo litawezekana kama tutafanya maunganisho kwa wateja wengi na ili kutoa huduma zaidi Dawasa tutaanza kutembelea maeneo wateja walipo ili kuweza kuwasogezea huduma zaidi kwa ukaribi,"

Hata hivyo, Katwiga ameeleza kuwa chanzo cha maji kina uwezo mkubwa wa ambapo kwa saa Lita za ujazo 284,500 zinazalishwa sawa na Lita milion 6.8 kwa siku.

Mradi huo uliweza kuhusisha ujenzi wa Tanki la maji Lita 1.5 kituo cha kusukumia maji kutoka kwenye chanzo na ulazaji wa mabomba kwa urefu wa Km 65 na wanufaika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo ni wananchi katika Vijiji vya Mkwalia Kitumbo, Kididimo, Sunguvuni na Kiguza wa kata ya Mkuranga huku Kata ya Kiparang'anda ni Kiparang'anda A, Kiparang'anda B na Magoza.

Mhandisi wa Miradi Mkoa wa Kihuduma DAWASA Mkuranga Richard Katwiga akitoa maelezo kwa moja ya mafundi wakati wa kuyaruhusu maji yaanze kwenda katika mtandao ili kuyasafisha na kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa Mkuranga kupitia mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Bilion 5.6 uliohusisha na ujenzi wa tanki la lita Milion 1.5
Mhandisi wa Miradi Mkoa wa Kihuduma DAWASA Mkuranga Richard Katwiga akionesha na kutoa maelezo ya  chanzo cha maji kinachotumika katika mradi wa maji wa Mkuranga. Chanzo hicho kina uwezo wa kuzalisha lita za maji milion 6.8  kwa siku sawa na lita 284,500 kwa saa

Kituo cha kusukumia maji kikiwa katika hatua za mwisho za ukarabati. Pampu moja ikiwa tayari imeshafungwa.

 Tanki la Ujazo wa Lita Milion 1.5 likiwa limekamilika na kuanza kupokea maji kutoka chanzo kilichopo Kijiji cha Mkwalia Kitumbo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...