Naibu Waziri wa maji Maryprisca Mahundi kulia akifungua koki katika mradi wa maji wa Kipapa na Mhilo uliotekelezwa na wakala wa maji vijijini Ruwasa mkoa wa Ruvuma ambao umewezesha wakazi wa kijiji ch Kipapa katika halmashauri ya wilaya ya Mbinga kuondokana na kero ya maji safi na salama iliyokuwepo kwa muda mrefu.


Naibu Waziri wa Maji MaryPrisca Mahundi amefanya ziara ya kikazi Wilayani Mbinga mkoani Ruvuma kwa kukagua miradi ya maji ya mabilioni ya fedha.

Katika ziara hiyo Mahundi amekagua mradi wa maji wa Kipapa na Mhilo ambao umetekelezwa kwenye Kata za Kipapa na Langiro, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wenye thamani ya shilingi Milioni 647.4

Mradi huo umekamilika na umeanza kuhudumia wananchi kwa kutoa maji safi na salama.

Naibu Waziri wa Maji pia ametembelea na kukagua miradi mingine miwili ya maji ambayo ni mradi katika Kijiji cha Lifakara unaokadiriwa kugharimu Shilingi Milioni 651 na mradi unaojengwa Kata ya Bethlehemu ambao unatarajia kugharimu sh.Bilioni 1.4 hadi kukamilika kwake.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa maji pia amekagua miradi ya maji inayotekelezwa kwenye vijiji vya Amani Makolo, Mabuni, Luhagara na Litumbandyosi wilayani Mbinga.

Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo Naibu Waziri wa Maji ametoa mwezi mmoja kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Ruvuma(RUWASA) kuongeza vituo vya kuchotea maji kwenye kitongoji cha Kiosi, Kijiji cha Kipapa.

“RUWASA hakikisheni mnaanza utekelezaji wa mradi wa kusambaza maji kwenye Kijiji cha Langiro Asili, Kata ya Langiro ndani ya kipindi cha miezi mitatu ijayo’’,alisisitiza Mahundi.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshongwa ametoa rai kwa wananchi kutunza vyanzo vya maji sanjari na miundominu ya maji iliyopo kwenye maeneo yao ili miradi hiyo iweze kudumu kwa muda mrefu na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...