Muwakilishi Kutoka Kampuni ya 361 Degree Benedict Msofe  akizungumza na Waandishi Wahabari Dar es salaam baada  kutangaza rasmi Uzinduzi wa Tuzo za Harusi kwa mwaka huu.
Muongozaji wa kampuni ya Innvex, Upendo Fatukubonye akitolea ufafanuzi wa jinsi ya upigaji kura na kueleza kuwa mchakato huo utakuwa wa haki na huru katika kuwapata washindi kwenye vipengele 20 na washiriki 65 watakaopatikana Mei mwaka huu. 

    Na Khadija Seif, Michuzi Tv

 MCHAKATO Wa Tuzo za Wauzaji na Watoaji Huduma za Harusi maarufu Kama "Harusi Awards" lazinduliwa rasmi.

Akizungumza na Waandishi Wahabari Muwakilishi Kutoka Kampuni iliyoandaa Tuzo hizo 361 Degree Benedict Msofe  amesema ni Wazi Kuwa Sherehe ni moja ya eneo ambalo Linatoa Fursa Mbalimbali .

"Sherehe ni moja ya eneo pana ambalo Watu wengi hujipatia kipato kwa sababu ya Mahitaji ya eneo husika,Sherehe itahitaji Chakula,Mapambo,Muziki,Mavazi na Kadhalika."

 Msofe ameeleza Sababu ya Kuanzishwa Kwa jukwaaa la Tuzo za Harusi ni kutunuku ufanisi na ubora kwenye Sekta ya Harusi.

Aidha,Msofe ameweka wazi Maandalizi ya Tuzo hizo na Mpaka sasa Takribani ya  Washiriki 65 katika Vipengele 20 Watawania Tuzo za Jukwaa la Harusi Kwa Mwaka huu ambapo zinatarajia Kufika kilele Mei 16 Katika Ukumbi Wa Serena hoteli huku kilele cha upigaji wa kula mwisho Mei 13.

Miongoni Mwa vipengele hivyo ni pamoja na Saluni bora,mpakaji makeup bora,Mapambo bora,Mshonaji bora,Mpishi bora wa Keki,Mpishi na Muandaaji wa Chakula kizuri na Vipengele vingine Vingi.

Kwa upande wake  Mdhamini Wa Tuzo hizo  Upendo Fatukubonye  Kutoka Kampuni ya Uhakiki Usalama data pamoja na Mifumo ya Makampuni amesema Kazi yao kuu itakua ni Kuendesha Mchakato wa kupata Kura Kwa haki bila upendeleo kupitia tovuti husika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...