Na Jusline Marco-Arusha

Kutokana na changamoto ya uhaba wa maji safi na salama kudumu kwa muda mrefu katika Kata ya Mwandeti,pamoja na changamoto nyingine za kimiundombimu,Serikali itaendelea kutatua changamoto hizo kwa kutoa fedha kadri zitakapopatikana kulingana na mahitaji yaliyopo katika shule ya sekondari ya Mwandeti iliyopo Wilayani Arumeru.

Akimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha katika maafali ya 4 ya kidato cha 6 yaliyofanyika kwenye shule hiyo,Mkuu wa shule ya sekondari Ilboru,Mwl.Denis Otieno amesema kupitia mradi mkubwa wa maji unaoendelea katika kijiji cha Losikito kilichopo ndani ya kata hiyo amesema mradi huo utakapokamilika tawi moja litaekekezwa katika shule hiyo ili kuweza kutatua changamoto hiyo.

Aidha alisema pamoja na serikali kuendelea kutatua changamoto hizo pia iliweza kutoa fedha za kukamilisha bwalo,maktaba na choo cha matundu 4 ambapo itakuwa inaendelea kutatua changamoto zilizopo shuleni hapo ili kukamilisha ujenzi wa mabweni yaliyobaki pamoja na nyumba za walimu.

Alieleza kuwa matokeo mazuri katika shule hiyo wapo watu ambapo waliumia kuhakikisha shule hiyo inafanya vizuri na wanafunzi wanakuwa na uelewa wa kile wanachofundishwa ambapo alimpongeza mkuu wa shule hiyo na kusema kuwa serikali inatambua mchango wake katika ukuaji wa elimu shuleni hapo.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa shule hiyo Mwl.John Massawe amesema kuwa pamoja na changamoto zilizopo shule hiyo haijawahi kutoka ndani ya 10 bora kutoka na wanafunzi wenyewe kujitambua,juhudi za walimu pamoja na uongozi wa wilaya kuhamasisha wanafunzi hao kusoma kwa bidii hivyo kupelekea matokeo kuwa mazuri.

Mwl.Massawe aliongeza kuwa tatizo la maji safi na salama katika shule hiyo limekuwa tatizo kubwa ambapo hulazimika kutumia shilingi laki mbili na arobaini kwa boza moja la maji ukilinganisha na idafi kubwa ya wanafunzi iliyopo maji hayo hayakidhi mahitaji hivyo changamoto hiyo huleta hasara kubwa katika uendeshaji wa shule.

Pamoja na changamoto hiyo pia Shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa nyumba za walimu kwani zimekuwa hazikidhi mahitaji ya walimu 43 ambapo mpaka sasa walimu wanaokaa shuleni ni walimu 9 hali inayopekelea walimu wengi kulazimika kuishi mbali na eneo la shule hiyo.

Naye mmoja wa wanafunzi Vedastina Jovenal katika hafla hiyo kwa niaba ya wanafunzi wenzake,alisema wamefanikiwa kukuza nidhamu ya shule kwa kutoa ushauri wa wadogo zao katika kipindi ambacho wamekaa shuleni hapo pamoja na kujiunga na mashirika mbalimbali likiwemo shirika la KISA ambalo linajihususha na ufundishaji wa mabinti namna ya kujitegemea na kutatua changamoto zao.

Awali akizungumza kwa niaba ya wazazi,Bwn.Thomas Ndaluka amewapongeza wazazi na walimu kwa ushirikiano walionao katika kuwalea watoto hao kimaadili na kitaaluma hivyo amewataka wazazi kutokuwa na mashaka nao wakati watakapofanya mitihani yao ya kuhitimu elimu yao.

"Kwa kweli walimu niwapongeze walimu kwa niaba ya wazazi wenzangu mmefanya kazi kubwa ya kuwapika wanafunzi na wakapikika vyema kitaaluma naamini watoto wetu hawatatuangusha katika matokeo."Alisema mzazi huyo

"Kwa niaba ya wazazi niendelee kuwapongeza pia ninyi wanagunzi kwa kuwa mmejitambua ,mmekuwa na mnafanya bidii katika masomo yenu vizuri na kuiweka shule katika nafasi nzuri ya kusifiwa,kinachofuata ni nyie kujiamini kwamba mnaweza na sina shaka na hilo kwa sababu mmesema wenyewe kuwa mtafanya vizuri."Aliongeza mzazi huyo

Vilevile aliwataka wanafunzi hao kuendelea kujifunza kwani katika kujifunza hakuna mwisho ambapo amewataka waendelee kujifunza na amewakaribisha katika kujiunga na vyuo vikuu kwa fani mbalimbali tofauti na walivyojiwekea mtazamo kuwa wenye fani za sanaa hawawezi kusoma kozi nyingine tofauti na sheria.

Hata hivyo shule hiyo ilianzishwa mwaka 2004 ikiwa na wanafunzi 28 kwa sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1316 wavulana wakiwa 491 na wasichana 825 na imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo yake ya kila mwaka ambapo katika mwaka 2018 shule hiyo ilikuwa nafasi ya 1 kimkoa na nafasi ya 2 kitaifa,2019 ilikuwa ya 2 kimkoa naya 4 kitaifa huku mwaka 2020 ilikuwa ya 3 kimkoa naya 9 kitaifa lengo likiwa ni kuondoka daraja sifuri na kubaki katika ubora.

Mwalimu John Massawe,Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwandeti akitoa nasaha zake kwa wahitimu wa kidato cha 6 katika Shule hiyo kwenye hafla ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu elimu yao.
Wahitimu wa kidato cha sita kayika shule ya sekondari mwandeti iliyopo Wilayani Arumeru wakisikiliza kwa makini nasaha kutoka kwa mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha,Mwl.Denis Otieno katika hafla iliyofanyika shuleni hapo.

 Mkuu wa shule ya sekondari Ilboru,Mwl.Denis Otieno  akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha kwenye maafali ya 4 ya kidato cha 6 katika shule ya sekondari ya Mwandeti iliyopo Wilayani Arumeru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...