Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuwainua wakulima wa zao la Korosho nchini, Serikali imekutana na Taasisi za Kibenki na kukubaliana nazo kufungua akaunti ya pamoja kwa ajili ya kuwasaidia wakulima hao kuweza kufanya kilimo chao vizuri.

Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dodoma kati ya Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na wawakilishi wa mabenki hayo ambapo lengo ni kuwawezesha pia wakulima kupata pembejeo kwa wakati.

Akizungumza na wandishi wa habari, Naibu Waziri Bashe amesema amefanya kikao na Benki ya Equity ambayo imeonesha wazi nia yake ya kuwainua wakulima huku akiongeza kuwa Benki zingine ambazo zimeonesha nia hiyo na kukubaliana ni pamoja na Benki ya NMB na CRDB.

" Kama mnavyofahamu kwa muda mrefu tumekua tukiangalia njia ambazo zitawawezesha wakulima wetu kupata pembejeo kwa wakati na kwa gharama nafuu, kwa muda mrefu mazao haya ya kimkakati kama Korosho mkulima anaenda Benki anakopa fedha kwa ajili ya kununulia pembejeo lakini anaenda Benki anakopa kwa riba iliyopo kwa wakati huo.

Sasa sisi kama Wizara tulikubaliana tuje na mkakati wa kumpunguzia gharama mkulima kwenye sekta ya kilimo hivyo tumeona ili kuondoa changamoto hiyo tutumie chama kimoja cha ushirika katika kushughulika nazo," Amesema Bashe.

Amesema baada ya kuangalia mapato yaliyopo wameangalia uhitaji wa wakulima wa Korosho ambapo kama ni Pembejeo hivyo kuamua mahitaji yote ya sekta yachukuliwe pamoja na kutumia chama kimoja cha ushirika kutangaza zabuni na ili mzabuni apeleke dawa ni lazima chama kikakope fedha Benki na kitatakiwa kulipa riba ya asilimia 16 hadi 20.

Amesema au kama siyo chama kukopa basi mkulima mmoja mmoja akakope Benki  hivyo baada ya mkataba huo wazabuni watapeleka mikataba benki LC kutoka taasisi za fedha ambazo gharama yake ni asilimia mbili ya riba.

" Kwahiyo gharama kwenye pamba imekua ni asilimia mbili na mabenki yameshatoa zaidi ya Bilioni 36 lakini pia tunafanya hivyo hivyo kwenye korosho mwaka huu ambapo wakulima watagaiwa dawa bure na pembejeo zote bure za korosho ambapo sasa watarudisha gharama hizo kutokana na mjengeko wa bei  na tayari washakaa na wanunuzi wa korosho na wamekubaliana watachangia kweye mfuko huo.

Ukitazama kwa miaka mitatu iliyopita zao liliendelea kushuka kwa sababu mkulima hakua na uwezo na alikua hakopesheki hivyo tunachokifanya sisi kama Wizara ni kusimamia kufunguliwa kwa Escrow akaunti ambayo itakaa katika benki ambazo tumekubaliana  ,tunashukurubenki tatu nilizozitaja tushakubaliana nazo na mchakato unaofanywa na wizara hivi sasa ni kufungua akaunti hizo ambazo zitasimamia na Chama cha Ushirika na Bodi ya Korosho, " Amesema Bashe.

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza na wawakilishi wa taasisi za fedha ambao amefanya nao kikao ofisini kwake jijini Dodoma cha kuangalia namna ya kuwainua wakulima wa zao la korosho nchini.

Wawakilishi wa Taasisi za Fedha na watendaji wa wizara ya kilimo wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwenye kikao chao cha kujadili namna ya kuwainua wakulima wa zao la korosho nchini.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...