Charles James, Michuzi TV

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka jana imebaini mapungufu makubwa katika uanzishwaji na uendeshaji wa Tamasha la Urithi Sh Bilioni 2.09.

Katika taarifa yake aliyoitoa leo jijini Dodoma mbele y wandishi wa habari baada ya kuiwasilisha Bungeni, CAG Charles Kichere amesema amesema katika ukaguzi wake wa Tamasha la Urithi lililokua na lengo la kukuza utalii na Urithi wa kitaifa aliambiwa kamati iliyoundwa iliidhinisha bajeti ya Sh Bilioni 1.60 kwa ajili ya utekelezaji wa hafla hiyo lakini bajeti hiyo haikuwasilishwa kwa ajili ya ukaguzi.

CAG Kichere amesema ukaguzi wake umebaini hakukua na mpango wa utekelezaji wa tamasha hilo hivyo kutokana na kukosekana kwa mpango huo alibaini Wizara ya Maliasili na Utalii iliomba wakala zake nne kuchangia jumla ya Sh Bilioni Moja ambazo hazikua kwenye bajeti ili kuweza kufanikisha tamasha hilo.

Amesema ili kuongezea bajeti hiyo Wizara ya Maliasili na Utalii ilichangia Sh Milioni 299, Mfuko wa Tozo wa Maendeleo ulichangia Sh Milioni 270 ambapo jumla ya Sh Bilioni 1.57 zilipatikana ili kufanikisha utekelezaji wa tamasha hilo ambapo fedha zote hazikua kwenye bajeti ya Wizara na Taasisi husika.

" Wakati wa utekelezaji nilibaini Kituo cha Televisheni cha Clouds na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) walilipwa jumla ya Sh Milioni 629 na Sh Milioni 204 mtawalia kwa ajili ya kurusha matangazo ya tamasha la urithi hata hivyo hakukua na risiti za kielektroniki zilizotolewa kuthibitisha kupokelewa kwa malipo hayo.

Pia kodi ya zuio ya Sh Milioni 31 na Sh Milioni 10 kutoka Clouds na TBC haikukatwa katika malipo yaliyofanyika," Amesema CAG Kichere.

Amesema amebaini kuwa jumla ya Sh Milioni 487 zilipelekwa kwenye Tamasha la Urithi lakini hakukua na nyaraka zilizowasilishwa kwa ajili ya ukaguzi ili kuthibitisha matumizi hayo.

" Nilibaini matumizi ya Sh Milioni 585.5 yaliyolipwa na Mhasibu wa Mfuko wa Tozo ya Maendeleo ya Utalii bila ya kuwa na nyaraka toshelezi, hivyo nilishindwa kuthibitisha uhalali na usahihi wa malipo hayo.

Aidha nilibaini Wizara ya Maliasili na Utalii ililipa Sh Milioni 140 kwa kampuni ya Wasafi kwa ajili ya wasanii ambao wangetangaza utalii wa ndani katika mikoa sita ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Iringa na Dodoma lakini hakukua na mkataba wowote uliosainiwa kati ya kampuni hiyo na wizara hivyo kushindwa kuhakiki wigo wa kazi pamoja na huduma zilizotolewa na kampuni hiyo," Amesema Kichere.

Amesema kulikua na maagizo ya Waziri  wa Maliasili na Utalii (Hamis Kigwangala) yakielekeza malipo kwa kampuni ya wasafi, katika mahojiano na waziri huyo alikiri kuwa kampuni ya wasafi iliomba zabuni ya kutangaza tamasha hilo kwenye mikoa iliyotajwa na kutoa maagizo ya kufanya malipo hayo.

CAG Kichere amesema kuwa kiasi cha Sh Milioni 140 kikicholipwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kampuni ya Wasafi kufuatia maelekezo ya Waziri wake hakiendani na sheria za manunuzi ya fedha za umma.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...