Kaimu kamishina mwandamizi wa TANAPA kanda ya kaskazini Herman Batiho akifungua kongamano la vijana la kujadili wajibu wa vijana katika kudumisha amani kongamano lililofanyika mkoani hapo juzi.
Kaimu kamishina mwandamizi wa TANAPA kanda kaskazini Herman Batiho (kushoto,) akibadilishana mawazo na mkurugenzi wa shirika lisilola kiserikali PPVO Chamulio Martin Mara baada ya kufungua kongamano hilo(picha na Woinde Shizza, Arusha.)

Na Woinde Shizza, Michuzi  TV- ARUSHA

VIJANA wametakiwa kuilinda amani iliyopo  kwa kushiriki katika uhifadhi wa rasilimali  zilizopo  nchini pamoja na  kuhamasisha utalii wa ndani  ili uchumi wa nchi  uendelee kukuwa kwa kasi .

Hayo yamesemwa na kamishna mwandamizi wa shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) kanda ya kaskazini Herman  Batho  akizungumza katika kongamano la vijana lenye lengo la kueleza  umuhimu wa vijana katika kuendeleza shughuli za utalii lililofanyika jijini Arusha.

Alisema  kwa kuwa  vijana ni nguvu kazi kubwa  ya taifa wanapaswa kuilinda amani iliyopo kwa kulinda rasilimali zilizopo  nchini na  kuhamasisha utalii wa ndani ili pato la nchi   liendelee kukuwa zaidi kutokana na uwepo wa watalii wengi wanaotembelea hifadhi.

Alisema ni vyema kila mtanzania akajua na kujiuliza  ni kwa namna gani anaweza kuchangia kuendeleza sekta ya utalii haswa katika kipindi hiki ambacho  wageni wanaotoka nje ya nchi kuja hapa nchini wamepungua kutokana na nchi zao kufugwa (lockdown) uliyosababishwa  na uwepo wa ugonjwa wa Covid 19.

“tunatakiwa watanzania tuinuke tusilale tu kisa watalii kutoka nje hawaji kutembelea mbuga zetu basi na sisi tusiende kutembelea, tunatakiwa tuamke sisi kama sisi  tutembelee tuhamasishane  kutembelea hifadhi zilizopo hapa nchini ukizingatia gharama zake kwa sisi wazawa ni ndogo  sana ambazo mtanzania yeyote yule anaweza kuzimudu,watanzania tupo zaidi ya milioni 60 kulingana na sensa iliyofanywa hapo awali lakini ukiangalia ni wangapi wanaotembelea hifadhi zetu kwa kipindi kwa mwaka uliopita ni watanzania milioni moja laki tano tu ndio wametembelea jambo ambalo halirizishi kabisa “alibainisha Batho.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bunge la vijana wa jumuiya ya afrika mashariki Jemsi Leonadi alisema kuwa  wao kama vijana wamejipanga kuwahamasisha wananchi wote  kutembelea hifadhi zetu ili pato la nchi  liendelee kukuwa  na uchumi  uendelee kupanda zaidi .

Alisema kuwa tunapokuwa na rasilimali kikubwa zaidi kinachotakiwa ni kujitangaza zaidi  na kuhamasisha zaidi utalii wetu kwani tunapohamasisha utalii wetu wa ndani inasaidia hata vijana ambao hawana ajira kupata ajira  kwani pindi wageni wanavyokuja au watu wanavyotembelea hifadhi zetu ndivyo jinsi ajira zinaongezeka.

Aliwataka wananchi hususa ni vijana kuendelea kulinda rasilimali  tulizoachiwa na waasisi wa nchi  zikiwemo mbuga  za wanyama, wanyama wenyewe waliopo katika hifadhi zetu,milima, mapori yetu ya akiba, maziwa yetu pamoja na madini ambayo tunayo ili yaje yavisaidie vizazi vyetu vya baadae.

Aidha  aliwasisitiza wananchi kuendelea kuilinda amani ambayo tuliyonayo bila kuvurugwa na mtu yeyote kwani tunapoipoteza amani hii hatutaweza kufaidi vitu vizuri ambavyo tunavyo  na tulivyobarikiwa na Mungu  kuwa navyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...