KATIKA kuhakikisha Uwekezaji unaendelea kuwa imara hapa nchini wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) watembelea katika kiwanda cha kutengeneze Saruji cha Twinga Cement kilichopo Tegeta mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza katika kiwanda cha Twiga Cement, Meneja wa kanda ya Mashariki kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bevin Ngenzi amesema kuwa lengo kuu la kutembelea kiwanda hicho ni kujionea kwa uhalisia kinachoendelea kiwandani hapo, kuangalia mafanikio yao pamoja na kuangalia changamoto zinazowakabili ili waweze kuzitatua kama serikali.

"Kwa changamoto ambazo serikali inaweza kuingilia kati ili tuweze kuhakikisha uwekezaji wao unakuwa bora zaidi hapa nchini, waweze kupata faida, watu wetu waweze kupata ajira na serikali iweze kupata kodi zinazotokana na uwekezaji."Amesema Banzi

Akizungumzia kuhusu mafanikio ya Kiwanda Twiga Cement amesema kuwa mafanikio yanaonekana kwani kwa kipindi cha miaka 10 kilichopita walikuwa wanazaliasha toni milioni moja na laki mbili kwa mwaka lakini mpaka sasa wamefikia kuzalisha tani milioni mbili kwa mwaka.

"Hii inaonesha mafanikio makubwa katika uzalishaji wa Saruji hapa nchini kwani kiwango kilichoongezeka ni kikubwa ukilinganisha na miaka 10 iliyopita." Amesema Ngenzi.

Kuhusu changamoto ya Kiwanda cha Saruji cha Twiga Cement za kisera pamoja na Utoaji wa mizigo Bandari, Ngenzi amesema watazungumza na taasisi husika ili waweze kuzitatua changamoto hizo.

Hata hivyo Ngenzi amesema wafanyakazi wa Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kwa baadhi ya changamoto wataziwasilisha kwenye taasisi za serikali zinazohusika ili waweze kuzitatu ili kuwawezesha wawekezaji ili waweze kuleta maendeleo zaidi.

Kwa Upande wa Meneja Mauzo Kutoka kiwanda cha Saruji cha Twiga Cement, Injinia Danford Semenda amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita walifurahia mikakati iliyotolewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa sababu ya miradi aliyoileta kwani imesaidia kukuza soko la Saruji hapa nchini.

Amesema kwa sasa wameongeza katika uwekezaji wa utengenezaji saruji hapa nchini kwani watanzania wanajenga kwa saruji ya Twiga Cement pamoja na miradi inayoendelea kutekelezwa na serikali inatumia Saruji hiyo kujenga miradi.

Licha ya hayo Injinia Semwenda amesema kuna miradi mingine mitatu inaenda kutekelezwa na kiwanda hicho kwani miradi hiyo itagharimi kiasi cha dola za kimarekani milioni 15.

Hata hivyo ameiomba serikali iendelee kutoa ushirikiano ili waendelea kufanya uwekezaji hapa nchini kwani watanzania zaidi ya 1000 wananufaika kutokana na uwekezaji wa kiwanda cha Saruji cha Twiga Cement.

"Kiwanda cha Twiga Cement kwa mwaka huu kimeongeza kiwango cha utoaji gawio la serikali kutoka shilingi milioni 290 kufikia kutoa kiasi cha shilingi 360 hii inaonesha mafanikio makubwa katika sekta ya viwanda hasa kiwanda cha Saruji cha Twinga Cement.

Hata hivyo Injinia Semwenda amesema kuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kutatua changamoto walizonazo ili waendelee kuwekeza hapa nchini kwa manufaa ya maendeleo ya taifa pamoja na mwanamchi mmoja mmoja.
Meneja wa kanda ya Mashariki kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bevin Ngenziwakwanza kulia akizungumza mara baada ya kutembelea Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Twiga Cement leo Aprili, 2021.Meneja Mauzo Kutoka kiwanda cha Saruji cha Twiga Cement, Injinia Danford Semenda akizungumza na wafanyakazi  Kituo cha Uwekezaji (TIC) leo Aprili 16, 2021.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) wakitembelea kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Twiga Cement waliotembelea kiwanda hicho leo Aprili 16, 2021.

Baadhi ya Mitambo ya Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Twiga Cement.
Meneja Mauzo Kutoka kiwanda cha Saruji cha Twiga Cement, Injinia Danford Semenda akizungumza na wafanyakazi  Kituo cha Uwekezaji (TIC) leo Aprili 16, 2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...