NA VICTOR MASANGU, PWANI

SERIKALI Mkoani Pwani kwa kushirikiana  na wadau mbali mbali wa zao la Korosho wameazimia kwa pamoja kujenga ujenzi wa kiwanda kikubwa kwa ajili ya kuchakata zao la Muhugo ambacho kitajengwa katika eneo la Chailinze lililopo  halmashaurli ya Chalinze Wilayani Bagamoyo kwa lengo la kuwakomboa  wakulima  wa  zao  hilo  kuondokana na changamoto zinazowakabili katika upatikanaji soko.

 Maazimio hayo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata zao  la Muhogo  yamefanyika katika mkutano wa wadau wa zao la muhogo katika Mkoa wa Pwani ambacho kimeweza kuwajumuisha viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wadau wa zao hilo wakiwemo wakulima kwa lengo la kuweka mikakati na kujadili  changamoto  zinazowakabili wakulima hao wa zao la muhugo.

Akizungumza  katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo ambaye alikuwa ni mwenyekiti  katika  mkutano  huo  alisema kwamba  lengo   kubwa serikali ni kuweka mikakati madhubuti ambayo itawasaidia kuwakomboa wakulima  wa zao la muhogo hivyo ujenzi  wa kiwanda hicho utakuwa ni mkombozi mkubwa na chachu ya kuleta  mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

 Alisema ,zao la Muhogo ni moja ya zao muhimu na kwamba likitumika vizuri linaweza kuwaongezea wakulima kipato na hata kuongeza kipato cha Mkoa na hata kujenga uchumi wa Taifa.

 

Ndikilo ,alisema kuwa wakulima wengi wanalima zao hilo huku wakiwa hawana utaalamu  wala elimu ya kutosha juu ya zao hilo na kwamba ni wakati wa maafisa ugani kuona namna ya kuwatembelea wakulima kwa kuwapa elimu ya zao hilo.

 

Aliongeza kuwa,mkoa wa Pwani unajumla ya hekta 3,353,900 ambapo eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 1,933,224 sawa na asilimia 57.66 ya eneo lote.

 

Alisema, pamoja na kuwepo kwa ukubwa wa eneo hilo lakini bado Muhogo hulimwa kwa kiasi kidogo ikiwa ni wastani wa hekta 60,703 na kuzalisha tani 500,000 hadi 650,000 kwa mwaka huku akisema eneo hilo ni asilimia tatu.

 

 " Kwa upande wa tija  nayo ipo chini kwa miaka mitano iliyopita uzalishaji kwa eneo ni wastani wa tani 6.5 hadi 7.6 kwa hekta  ingawa yapo maeneo machache hasa Kibiti na Rufiji ambako tija ni kati ya tani 9 hadi 18 kwa hekta wakati tija inayopendekezwa kitaalamu kuwa ni tani 20 kwa hekta" alisema Ndikilo.

 

Kuhsu usindikaji mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa  bado haufanyi vizuri pamoja na kuwepo kwa juhudi za kuanzisha vikundi na Viwanda vya usindikaji kwani vikundi 32 vilivyopo katika Mkoa huo havisindiki mihogo kwa madai ya kukosa soko la uhakika.

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Wadau wa Zao la Muhogo (TACAPPA) Mwantumu Mahiza, alisema endapo wakulima watahamasishwa kuhusiana na zao hilo litawasaidia kujikwamua kutoka kwenye umasikini.

 

Mahiza, alisema maaofisa ugani wanatakiwa kusaidia kutoa elimu kwa wakulima ili waweze kulima zao hilo kitaalamu na kupata mbegu bora na kwamba bila hivyo hakuna mafanikio yatakayopatika.

 

Alisema,chama hicho kimejipanga kupambana na vikwazo vya soko la zao hilo ambapo vikitolewa wakulima watachangia kuinua uchumi wa taifa na kuondoa umasikini wa kaya.

 

Mahiza,alisema kuwa kwasasa Taccapa kipo katika mpango wa kujenga kiwanda kikubwa cha Muhogo ambacho kitahudumia Mikoa ya Kanda ya Mashariki na Kati na kufanya Muhogo kupata soko kubwa zaidi.

 

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dkt.Dolphine Magere,alisema kuwa kikao hicho kinalenga kutoa dira ya kuhakikisha zao Muhogo linapata hadhi kama mazao mengine.

 

Magere,alisema baada ya kikao hicho timu mbalimbali kupitia Halmashauri zitaundwa kwa kuwashirikisha maafisa ugani ili kusudi wawe karibu na wakulima wa zao hilo.

 

Mmoja wa wakulima aliyeshiriki kikao hicho Gosbert Joshua  aliomba kuwepo na kituo cha kuzalisha mbegu za Muhogo kuondoa usumbufu wa kuzifuata mbali na wanapoishi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo akizungumza  katika mkutano wa wadau wa zao la muhogo katika Mkoa wa Pwani ambacho kimeweza kuwajumuisha viongozi mbali mbali wa serikali, wakulima na taasisi binafsi kushoto kwake ni Katibu Tawala wa  Mkoa  wa  Pwani Dk. Delphine Magere na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa mstaafu Mwantumu Mahiza.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani mstaafu Mwantumu Mahiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la wazalishaji na usindikizaji wa mihogo Tanzania ( TACAPPA)  akizungumza na wadau mbali mbali wa zao la muhogo pamoja na viongozi wa serikali kujadili mambo mbali mbali ya kuweka mikakati ya kuwasaidia wakulima.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere wa kulia akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Zamani ya Mkuranga wakiwa wanafuatilia mada mbali mbali ambazo zilikuwa zinatolewa katika kikao hicho cha wadau wa zao la korosho.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarits Ndikilo akiwa anasisitiza jambo kwa wadau wa zao la korosho pamoja na viongozi wa serikali  wakiwemo wakulima ambao walihudhulia katika mkutano huo wa kujadili zao la korosho.
Mkuu wa Wilaya ya Kisaarawe Jokate Mwegelo akiwa anafuatilia jambo pamoja na viongozi mbali mbali na wadau  wa korosho wa Mkoa wa Pwani.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU). 

 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...