Wananchi wa Kijiji cha Nyashige, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, kabla ya kukabidhi madawati yaliyochongwa na wnanchi hao kwa ajili ya shule ya msingi ya kijiji hicho.



Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, akizungumza na wanacnhi wa Kijiji cha Nyashigwe, Kata ya Chabura wilayani humo jana.



Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli (kulia), akiwakabidhi moja ya madawati yaliyotengezwa na wananchi wa Kijiji cha Nyashigwe, wanafunzi wa shule ya kijiji hicho, Patrick Costantine (kushoto), Kado Safari (wa pili kushoto) na Mwalimu Mkuu wao, Ishengoma Kabuche (wa pili kulia).Picha zote na Baltazar Mashaka

…………………………………………………………………………….

NA BALTAZAR MASHAKA, Magu

WANANCHI wa Kijiji cha Nyashingwe,Kata ya Chabula wilayani Magu, wakabidhi madawati 54 yenye thamani ya sh. milioni 2.7 kwa shule ya msingi ya kijiji hicho ili kutatua changamoto ya watoto kukaa chini.

Pia wamejenga maboma mawili ya madarasa na ofisi ya walimu kwa nguvu zao katika jitihada za kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani mradi ambao umegharimu sh.milioni 6.3.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho Devota Aloys alisema jana kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kalli, wakati akitoa taarifa ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa nguvu za wananchi kijijini humo.

Alisema kaya sita kila kitongoji za vitongoji vinne zimetengeneza dawati moja ambapo kitongoji cha Nyashigwe kimetengeneza madawati 9 kati ya 11,Kibambu 19 (bado 2), Nyamilomate 20 wanadaiwa moja 1 na Zuli 6 kati ya 8 hivyo madawati 54 kati ya 62 yamepatikana kulingana na mgawanyo wa kila kitongoji.

Aloys alisema madawati hayo yamepunguza uhitaji katika Shule hiyo ya Msingi Nyashigwe yenye wanafunzi 750 kutoka 146 hadi 84,ambapo ina madasara 7 kati ya 17 ili kukidhi mahitaji hivyo madarasa yaliyojengwa na wananchi yakiezekwa yatasaidia.

Pia alisema shule hiyo ina uhaba wa matundu 29 ya vyoo yaliyopo ni 6 kati ya 35 na kuiomba serikali iwasaidie kujenga vya kisasa ili kunusuru afya za wanafunzi na baada ya wananchi kujenga zahanati kwa nguvu zao na kukamilisha boma kwa sh. milioni 8 linahitaji kuezekwa.

Kwa upande wake Kalli alisema serikali lazima iunge mkono juhudi za wananchi na itaendelea kuboresha elimu baada ya kufuta ada kuanzia darasa la awali hadi sekondari kidato cha nne ili watoto wasome hasa wa kike na kwa heshima ya wananchi kwa kazi waliyoifanya atapeleka madawati 10 kwenye shule hiyo.

“Elimu ni bure na madawati haya yatawanufaisha watoto,hivyo wazazi muache tamaa ya maliwa, waacheni watoto wa kike wasome,ni tunu katika taifa letu na hapa watatoka makamu wa rais, naibu spika,mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu wanawake,kwanza ni waaminifu hawapindishi maneno kama wanaume,”alisema Kalli na kuwataka watoto wawaenzi wazazi na wananchi kwa kufaulu mitihani yao vizuri.

Pia aliahidi ifikapo Aprili 30,atapaua na kuezeka vyumba vya madarasa vilivyojengwa na wananchi hao na kumwagiza Meneja wa Tanesco Magu kwenda kwenye shule hiyo kupima nguzo zinazohitajika ili waunganishwe kwenye Mradi wa Umeme Vijijini (REA).

Aidha baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo,waliwashukuru wazazi na wananchi kwa kujitoa kwao na kuwajengea madarasa pamoja na kuwatengenezea madawati.

“Tunawashukuru wazazi kwa jitihada zao,wengi mavazi yalichafuka kwa tulikuwa tunakaa chini, pia tunamshukuru Hayati Rais John Magufuli kwa kutoa elimu bure na tutaendelea kumkumbuka kwa hilo,”alisema Bulala Simba.

Patrick Costantine yeye alisema madawati hayo yatakuwa kichochea cha kusoma kwa bidii ili wafaulu masomo na kutimiza ndoto zao huku Kado Safari akisema kuondolewa kwa changamoto ya kukaa chini wataongeza bidii ya kujifunza zaidi. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Ishengoma Kabuche, alisema uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa uliathiri utoaji wa taaluma na kushusha ufaulu, hivyo jitihada na mchango wa wananchi wa kuchonga madawati 54,ujenzi madarasa mawili na ofisi ya walimu kutaondoa msongamano wa wanafunzi darasan

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...