Na Emmanuel Massaka,Michuzi TV
WANANCHI wa Kata ya Tambani wilayani Mkuranga mkoani Pwani wamesema watamkumbuka sana aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati John Magufuli kwa kufanikisha kupatikana kwa daraja la kifaurongo linaloendelea kujengwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Tambani, Nassibu Makamba amesema eneo la Kifaurongo linalojengwa daraja ni korofi pindi mvua zinaponyesha na kusababisha wananchi kuvuka na madumu hali inayo hatarisha usalama wa maisha yao.

Amesema kukamilika kwa daraja hilo kutatua changamoto kubwa kwa wananchi wa tambani waliokuwa wakiipata mvu zinaponyesha ikiwa ni pamoja na kufungua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Ameongeza Tambani inategemea kwa kiasi kikubwa kupata mahitaji yake temeke kwa sababu ni jirani hivyo kukamilika kwa daraja hilo kutawaarahisisha wananchi kupata mahitaji yao kutoka temeke ambayo ni hospital na shule.

Aidha Mbaga amempongeza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega kwa kuwapigania mpaka kupatikana kwa daraja hilo ambalo linaendelea kujengwa, na kueleza hawatamsaahu hayati Magufuli kwa kufanikisha changamoto yao hiyo kutatuliwa.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wakizungumza walipokuwa kwenye eneohilo, wamemshukuru mbunge wa jimbo la mkuranga pamoja na hayati john magufuli kwa ujenzi wa daraja hilo, ambalo linajengwa kwa Mara ya pili baada ya kujengwa nakisha kubomoka kutokana navua za mwaka 2020.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Nasibu amewatoa hofu wanachi na kusema uwa atakama daraja hilo halitokamilika kwa wakati, lakini hatahakikisha kunapatika na kivuko cha dharura ili wananchi wapate kuvuka kwa usalama kipindi cha masika.
Kama inavyoonekana pichani Mafundi wakiendelea na kazi leo ya kujenga daraja Kifaurongo lilipo kata ya Tambani wilya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.


Kama inavyoonekana pichani Mafundi wakiendelea na kazi leo ya kujenga mitaro barabara ya Vianzi Sangatini kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
(Picha zote,Emmanuel Masssaka wa Michuz Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...