JAMII ya watanzania imetakiwa kupanda miti ya tiba lishe kwa ajili ya kupata  tiba asili kutokana na magonjwa mbalimbali ambayo yanayowakumba.

Rai hiyo imetolewa jana na Mtafiti Mwandamizi Dr. Mary Maige kutoka Kituo cha Taasisi ya  utafiti wa magonjwa ya Binadamu na Tiba (NIMRI) wakati wa maadhimisho ya siku maalumu ya upandaji miti lishe yaliyofanyika katika Kijiji cha Makumbusho ya Taifa kijitonyama Jijini Dar es salaam.

Dr. Mary ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NIMRI katika maadhimisho hayo alisema kwamba mazingira yanahitaji kutunzwa kwa ajili ya Maisha ya Binadamu kama vile kusaidia tiba na pamoja na lishe.

"Tunahitaji kutunza mazingira ili nasisi yatutunze , tupande miti na kuhifadhi miti ili tuweze kutumia katika kutibu magonjwa mbalimbali, pia kuweka nguvu za ziada kutunza na kuhifadhi mazingira kutokana na sera ya Viwanda tunayoitekeleza kwa sasa" alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dr Noel Luoga alisema kwamba wanahamasisha jamii kupanda miti kwani inasaidia katika mambo mbalimbali muhimu katika maisha yao.

Dr.Luoga alisema kwamba misitu inasaidia katika mambo ya kiuchumi pamoja na maisha ya kibinadamu ikiwemo masuala ya tiba asili , mila na desturi kama vile kufanya matambiko na mambo mengine hivyo haina budi kutunzwa.

"Sisi kama Makumbusho ya Taifa tunaanzisha programu ya upandaji miti endelevu ili kusaidia kuelimisha jamii kujua umuhimu wa kupanda miti pamoja na kuthamini misitu kwa ajili ya Maisha ya kila siku " alisema.

Akizungumza muhifadhi wa misitu wilaya ya Kinondoni Dotto Ndumbikwa kutoka Mamlaka ya uhifadhi wa misitu nchini TFS alisema kwamba TFS ina bustani kubwa iliyopo Mwandege kwa ajili ya kusambaza miche mbalimbali ya miti katika mkoa wa Dar es salaam.

Alisema kwamba Mamlaka hiyo imetoa miche mbalimbali ambayo imepandwa katika shamba darasa lililopo Kijiji Cha Makumbusho ikiwa Ni kutoa elimu ya umuhimu wa upandaji miti na kuhifadhi mazingira huku akitoa wito kwa Jamii kupeleka maombi ili wapatiwe miche kwa ajili ya kupanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...