Kalamu ya Twende pamoja, Matokeo ya Haraka.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natumai mmeitikia kwa sauti kubwa "Kazi iendelee".

Naam kazi nzuri iendelee ya kumalizia miradi ya kimkakati; kazi iendelee ya kukuza uchumi; kazi iendelee ya kupambana na maadui ujinga, maradhi na umaskini; kazi iendelee ya kupambana na rushwa na ufisadi. Kama ni upele umempata mkunaji, Rais Samia.

Hatuwezi kumtenga Rais wa sita awamu ya 5 Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kazi nzuri iliyokwisha fanyika hapo awali, alikuwa sehemu ya kazi kubwa iliyokwisha fanyika.

Sasa ni wakati ambapo ni Rais kamili, Mhe. Samia kuhakikisha kazi kubwa iliyokwisha fanyika inaleta matokeo ya haraka sasa na yanayogusa na kuakisi maisha ya Watanzania.

Twende sawa hapa. Watanzania wamevumilia kuona matrilioni ya kodi zao zikielekezwa kwenye miradi ya kimkakati, wanataka kupitia kwa Rais Samia waone matokeo ya kodi zao. Mathalani, ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR ikikamilika na waanze kusafiri kwa unafuu, haraka na kwa muda mfupi; Watanzania wanataka kuona mradi wa maji wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ukizalisha megawatts 2115 na wapate umeme wa uhakika na wa gharama nafuu. Ni suala la matokeo ya haraka sasa yanahitajika ambayo hatuna shaka Rais Samia anatosha kufikisha matarajio ya ndoto za Watanzania.

Watanzania wanataka matokeo ya haraka sasa ya kuendelea kuwakomboa wanyonge kuhakikisha umeme wa REA unafika Tanzania nzima kwenye vijiji vyote salia; kuimarisha upatikanaji wa mbolea; kuendeleza wachimbaji wadogo; kusimamia upatikanaji wa mikopo na ulinzi wa biashara za Wamachinga, Mama Ntilie, bodaboda kote nchini.  Watanzania hatuna shaka Rais Samia anatosha kabisa kuendeleza ukombozi wa Wanyonge hawa ili kupitia matokeo ya haraka sasa yaonekane kwao ili wasiitwe tena Wanyonge.

Mifano ni mingi na maeneo tarajiwa ya kuhitaji matokeo ya haraka sasa ni mengi. Itoshe kusema,  Watanzania wanataka kuona matokeo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, malengo ya 2025 yakitimia na kuleta matokeo ya haraka tarajiwa.

Huu si wakati wa vijembe, kujimwambafy, kunyosheana vidole bali ni wakati wa kusonga mbele kwa imani, umoja, mshikamano, ushirikiano kwa malengo yale yale ya matokeo ya haraka sasa kupitia kwa nahodha wetu shupavu, jasiri, hodari, mzalendo na mchapa kazi, Rais Samia.

#TwendePamoja
#MatokeoYaHarakaSasa
#QuickResultsNow (QRN)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...