Na Mwandishi Wetu,Michuzi Blog

CHAMA Cha Mapinduzi( CCM) kimewapongeza na kuwashukuru wanachama, viongozi wa  Chama na Jumuiya zake, Wabunge, Viongozi wa Serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Wananchi wa majimbo ya Buhigwe na Muhambwe sambamba na Kata zilizofanya uchaguzi, kwa kukamilisha kwa salama, amani na mafanikio makubwa chaguzi ndogo zilizokamilika Jana Jumapili Mei 16, 2021. 

Katika chaguzi hizo, wagombea wa CCM jimbo la Buhigwe Ndugu Felix Kavejuru alitangazwa mshindi kwa kura 25,274 sawa na asilimia  83.3 ya kura zote na Jimbo la Mihambwe Ndugu Florence Samizi ameshinda kwa kura 23,441 sawa na asilimia asilimia66 pamoja na wagombea wa CCM katika Kata 17 wametangazwa kushinda  kwa kishindo.

Kupitia iliyotolewa leo Mei 17,2021 kwa vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka amesema ushindi huo mkubwa ambao wameupata kwenye majimbo ya Buhigwe na Muhambwe pamoja na Kata 17 ni zawadi ya wanaCCM kwa Mwenyekiti wao Samia Suluhu Hassan. 

Pia, wananchi hasa wa Kigoma wakimshukuru kwa kumteua mtoto wao Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

"Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, anatoa shukrani kwa makada wa CCM, viongozi wa Mkoa wa Kigoma, Jumuiya za Chama ngazi ya Mkoa na Taifa waliohakikisha ushindi wa CCM unapatikana. 

"Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kujisahihisha, kujiimarisha na kuwahakikishia Watanzania kuwa Ilani ya uchaguzi wa CCM 2020-2025 itatekelezwa kwa mafaniko makubwa katika maeneo yote kiuchumi, kijamii na kisiasa,"amesema Shaka.

Aidha amesema CCM itaendelea kusimamia na kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa vyama vyote kufanya siasa safi zenye tija za kuwaunganisha watanzania ili Taifa lizidi kupiga hatua za kimaendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...