Costantine Magavilla (wa tatu kulia) ambaye ni moja ya waratibu na waandaaji wa Tamasha la Sanaa za sakarasi kupitia Circus Mama Afrika ambalo litafanyika Mliman City jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 13 hadi Mei 16 akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo.
Mmoja ya wasanii wa sanaa za sakarasi Asha Mohamed (wa pili kulia) akizungumzia jinsi ambavyo wamejiandaa kutoa buradani kw watanzania kupitia tamasha ambalo linatarajia kufanyika Miman City jijini Dar es Salaam ambapo ameomba wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia buradani ya sarakasi yenye viwango vya kimataifa.
Mratibu na mdau wa tamasha hilo Costantine Magavilla (wa tatu kulia) akifafanua jambo kuhusu tamasha la sarakasi ambalo litafanyika Mliman City jijini Dar es Salaam ambapo kiingilio kitakuwa Sh.20,000 kwa wakubwa na Sh.15000 kwa watoto.








Picha mbalimbali za wasanii wa sarakasi kutoka Circus Mama Afrika wakiendelea kujinoa kwa ajli ya tamasha ambalo linatarajia kuanza kufanyika Mei 13 hadi Mei 16 katika eneo la Mliman City jijini Dar es Salaam.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

WANANCHI wa Jiji la Dar es Salaam wameombwa kutenga muda wao kwa ajili ya kufika kwenye maonesho ya tamasha la Eid ambapo kutakuwa na burudani za sanaa ya sarakasi ambayo imeandaliwa na CIRCUS Mama Afrika.

Tamasha hilo la maonesho ya sanaa nayatarajia kufanyika kuanzia Mei 13 hadi Mei 16 mwaka huu katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam na kiingilio kitakuwa Sh.20,000 kwa wakubwa na Sh.15 kwa watoto na kwa siku litakuwa likifanyika mara tano.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Mmoja ya waratibu wa tamasha hilo Costantine Magavilla amesema kwamba kila onesho litafanyika kwa dakika 70 bila mapumziko na muda wote wasanii wa sanaa ya sarakasi kutoka Circus Mama Afrika watakuwa wakitoa burudani yenye kiwango cha kimataifa.

"Buradani ya sanaa za sarakasi itatolewa kutoka kwa vijana wetu wa Kitanzania ambao wamebobea kwenye tasnia ya sanaa ya sarakasi, wanauzoefu wa kimataifa.Hakika wale ambao watakuja kwenye tamasha hilo hawatajutia kwani watapata buradani yenye kiwango cha juu, iwe mkubwa au mtoto atafurahia,"amesema Magavilla.

Akieleza zaidi kuhusu tamasha hilo kulifanya kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Eid, Magavilla amesema wananchi wengi kipindi cha Eid wamekuwa wakitafuta maeneo ya kwenda na kupata burudani rafiki kwa ajili ya familia nzima.

"Hivyo kwenye maenesho hayo ni burudani tosha kwa yoyote atakayekuja kuhudhuria , kama wewe ni mtu mzima, kijana au mtoto  mtapata buradani tosha kwa kuwa maonesho haya yamezingatia kiwango cha kimataifa.Maandalizi yote kwa ajili ya tamasha hilo yamekamilika kwa asilimia 100 na kilichobakia ni wananchi kuja kushuhudia kile ambacho tumewaandalia kipindi hiki,"amesisitiza Magavilla.

Aidha amesema kwa sasa tamasha hilo linafanyika eneo hilo la Mliman City jijini Dar es Salaam, hivyo rai yake kwa wananchi kuhakikisha wanafika kupata buradani kwani tamasha la sarakasi lenye kiwango cha kimataifa hufanyika kwa nadra sana.

"Kwa wakazi wa Dar es Salaam kama kama unataka kuona haya maonesho basi ni kwa siku hizo nne zilizopo mbele yetu na huko mbeleni hatujui yatakuwa wapi huenda yakawa mikoani, hivyo kwa wale wa Dar es Salaam huu ndio wakati wao, tunawakaribisha waje wapate burudani,"amesema.

Kuhusu usalama, amesema kiasili eneo la Mliman City lina usalama wa kutosha lakini Circus Mama Afrika katika kuhakikisha wanaohudhuria wanakuwa salama, wameweka usalama wa ziada ili kuhakikisha watakaofika basi wanaondoka wakiwa salama wao na mali zao.

"Usalama kama mnavyoona eneo la Mliman City lina usalama wa kiwango cha juu kwa maana zote kwa maana ya usalama wa watembea kwa miguu, usalama wa magari na hakuna matukio ya uhalifu kama maeneo mengine,"amesema Magavilla.

Mmoja ya wasanii wa sarakasi na dansa Asha Mohamed ametumia nafasi hiyo kusisitiza kuwa wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kutoa buradani, hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi na hawatajutia kwa kiasi cha fedha ambacho watakitoa kwa ajili ya kiingilio katika tamasha hilo.

"Tunawakaribisha  watanzania wote na wageni , ambao watatoka katika nchi mbalimbali ambao watakuwa hapa nchini katika kipindi hiki cha sikukuu ya Eid , tunawaambia tumewaandalia vitu vizuri na watakaofika watafurahia,"amesema Asha.

Ameongeza ni mara chache kufanyika kwa maonesho ya sarakasi kufanyika nchini, hivyo ametoa ombi kwa wananchi kufika kujionea vipaji walivyonavyo wasanii wasarakasi wa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...