Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU Ludovick Utouh akizungumza wakati wa kuwasilisha mada katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dodoma kwa kuwakutanisha wadau kutoka Asasi za kiraia kujadili na kuichambua ripoti ya CAG.
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh (kulia) wakisikiliza michngo mbalimbali na maswali kutoka kwa wadau walioshiriki kwenye mkutano huo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga akizungumza wakati wa kufungua wa Jukwaa la wakurugenzi jijini Dodoma.


Wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, wadau kutoka CSOS na Kamati za Bunge walishiriki kwenye mkutano huo.


Na Mwandishi Wetu

FOUNDATION for Civil Society (FCS) kwa kushiriana na WAJIBU Institute of Public Accountability kupitia Jukwaa la Wakurugenzi wa Asasi za Kiraia Nchini  kwa pamoja wamekutana jijini Dodoma kujadili Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 Katika kuboresha utendaji kazi.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo ulioashirikisha wadau mbalimbali  Mkurugenzi Mkuu wa Foundation for CIvil Societ Francis Kiwanga amesema lengo la mkutano huo ni kuweza kupata uchambuzi wa Taarifa hiyo na  kuchukua hatua ili kuboresha uwajibikaji na uwazi katika kuboresha  utendaji  kwa Serikali.

"Kila mwaka huwa tunakutana kujadili taarifa za ukaguzi wa hesabu za serikali lengo likiwa ni kuongeza nidhamu na kudhibiti ubadilifu wa rasilimali za Serikali na kupitia maajadiliano hayo tutakuwa na jambo moja katika kuimarisha utendaji kazi wetu"amesema Kiwanga.

Ameongeza kama asasi za kiraia wamekuwa wakifanya kazi na Serikali ili kuwasaidia wananchi katika suala zima la uwazi na uwajibikaji  kwa maslahi mapana ya Nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU  Ludovick Utouh ambaye pia ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Mstaafu ambapo Taasisi yake ndiyo iliyofanya uchambuzi wa Ripoti hiyo amempongeza CAG Charles Kichere kwa Ripoti nzuri yenye jumla ya Ripoti 21.

Utouh aliyekuwa akiwasilisha mada kwa wadau hao, amesema kumekuwepo na suala la kuongezeka kwa hati chafu na kwamba suala hilo linaonesha kuwepo na shida katika suala la Mahesabu huku akieleza kuwepo kwa udhaifu katika ukaguzi wa ndani.

Aidha amewaomba wananchi kuhakikisha wanaimarisha masuala ya uwazi na uwajibikaji katika kuikosoa Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...