Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) leo alfajiri Mei 8, 2021 imezindua rasmi safari za ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou nchini China.
Uzinduzi huo uliofanyika kwenye Jengo Namba 3 la abiria (terminal III) katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere umeongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi. Ladislaus Matindi.


Kwa mujibu wa ATCL, safari kati ya Dar es Salaam na Guangzhou itatumia saa 11 na zitakuwa safari pekee za moja za moja kwa moja kati ya maeneo hayo mawili.


Tangu mwaka 2015 serikali imewekeza nguvu katika kufufua kampuni hiyo ambapo jitihada hizo ni pamoja na kununua ndege, kukarabati na kujenga viwanja vya ndege na kuongeza rada za kuongozea ndege ili kuziwezesha ndege za shirika hilo kufika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho (katikati) kwa kushilrikiana na viongozi wa Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) wakizinduwa safari za ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou nchini China,mkoa wa Dar es Salaaam. (Picha na Emmanule Massaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...