Kikosi cha timu ya KMC FC.

MARA baada ya kutoka sare dhidi ya Namungo, Kikosi cha KMC FC kimendelea kujifua kuelekea katika mchezo wake mwingine wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Azam utakaopigwa siku ya Jumamosi Mei 15 katika uwanja wa Chamanzi.

Mchezo huo ambao KMC FC itakuwa ugenini, utachezwa saa 16:00 jioni ambapo hadi sasa kikosi hicho kinaendelea kufanya maandalizi yake ya mwisho ili kuhakikisha kwamba inakwenda kufanya vizuri katika mchezo huo muhimu.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni Chini ya Kocha Mkuu John Simkoko na msaidizi wake Habibu Kondo wameendelea kukiandaa kikosi hicho ili kuhakikisha kwamba ushindi unapatikana licha ya kuwepo na ushindani kwa timu zote mbili mkubwa na hivyo kuondoka na alama tatu muhimu.

”Tumetoka kwenye mchezo ambao tulikuwa ugenini dhidi ya Namungo, na sasa tunajiweka tayari kwenye mchezo mwingine, tunakutana na Azam FC ambayo kimsingi ni bora, inauwezo mkubwa, lakini hata ukiangalia kikosi chetu kiko bora zaidi, na kikubwa tunakwenda kupambania alama tatu ambazo hata wao wanazihitaji.

Ukiangalia hata kwenye msimamo wa Ligi, wapo nafasi ya tatu na sisi tupo kwenye nafasi ya tano, lakini pia katika mchezo uliopita tulipata ushindi wa goli moja tukiwa kwenye uwanja wetu wa nyumbani, hivyo licha ya kwamba tunaenda ugenini bado tunajiamini kwakuwa tunauwezo mkubwa wa kupambana na yoyote kwa ajili ya maendeleo ya Timu yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...