Na Mwandishi wetu, Dodoma
NAIBU
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, mhe Pauline Philip Gekul
ameipongeza timu ya soka ya wanawake ya Simba Queens kwa kutwaa
ubingwa wa ligi kuu ya wanawake (Serengeti Lite Women Premier League).
Mhe
Gekul akizungumza jijini Dodoma leo Jumatatu Mei 17 wakati timu hiyo
ilipotembelea Bungeni amesema Simba Queens imestahili kushinda ubingwa
huo kutokana na namna ilivyokuwa inapambana uwanjani kwenye michezo
yake.
"Nina wapongeza
viongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wote kwa juhudi kubwa
mlizoonyesha katika kipindi chote cha ligi na kuweza kuwa mabingwa kwa
mara ya pili mfululizo," amesema mhe Gekul.
"Ligi
ilikuwa na ushindani mkubwa lakini mmeweza kuibuka washindi, hii ni
ishara kuwa ligi yetu ya wanawake inazidi kuimarika," amesema mhe
Gekul.
Timu ya Simba
Queens imepata mwaliko maalumu wa kutembelea bungeni leo tarehe 17 Mei,
2021 mara baada ya kutwaa taji la ligi ya wanawake kwa kuifunga timu ya
Baobab Queens goli 1-0 katika mchezo uliofanyika jana kwenye uwanja wa
jamhuri jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...