Na,Jusline Marco,Arusha

Naibu waziri wa wizara ya katiba na sheria Geoffrey Mizengo Pinda amewataka wananchi na viongozi wote kutambia  kuwa takwimu sahihi za vizazi ni kichocheo kikubwa cha uchumi katika nchi kwani itasaidia serikali kupanga mipango yake ya maendeleo kwa usahihi.

Akizindua mpango wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Arusha na Manyara ,Pinda alisema katika sensa ya mwaka 2012 asilimia 13.4 tuu ya watanzania ndio WALIOKUWA wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.

Adha alitoa wito kwa mikoa yote nchini ambayo imeshafikiwa na zoezi hilo kuhakikisha wanaendelea kusajili kwani kila siku watoto wanazaliwa ikiwa ni pamoja na kuutaka mkoa wa Arusha na Manyara kuingia katika ushindani wa zoezi hilo na itakapofika wakati wa tathimini kila mmoja awe ametoa alipo na kuwa juu.

Sambamba na hayo Kampuni ya Tigo,Kanda ya Kaskazini imekabidhi simu za mkononi zipatazo 1350 zenye thamani ya shilingi milioni 169 kwa Mikoa ya Arusha na Manyara kwaajili ya kuwawezesha Wakala wa Usajili na Ufilisi RITA ili kuwezesha zoezi la usajili wa watoto walio chini ya miaka 5 kuweza kipata cheti cha kuzaliwa.

Akikabidhi simu hizo katika uzinduzi wa mpango wa usajili watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Arusha na Manyara uliofanyika jijini Arusha,Mkurugenzi wa kampuni ya mtandao wasimu Tigo Tanzania,Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo alisema kampuni ya inatambua kuwa nyaraka za awali za utambulisho wa mtoto ni cheti cha kuzaliwa hivyo wazazi na walezi wajitokeze kwa wingi ili kuweza kuwapatia vyeti hivyo.

"Kwa kushirikiana na wadau wetu RITA,Serikali ya Tanzania,Ubalozi wa Canada pamoja na UNICEF,kama kampuni ya Tigo tumeendelea kuwa RITA simu za kusajili watoto ambazo zinakuja na TEHAMA ya bure ambayo wanaweza wakaitumia na kuweza kutuma ujumbe kwa njia ya sms."Alisema Kinabo

Aidha alieleza kuwa Kampuni ya Tigo imefanikiwa kuonesha umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika zoezi hilo na wameendelea kuwekeza hivyo jambo hilo lipewe umuhimu ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa ambapo amewataka watumiaji hao wajifunze kuvitunda vifaa hivyo.

"Vifaa hivi tulivifanyia uhakiki kwamba vinaweza kufanya zoezi hili hivyo mtumiaji lazima ajifunze kuvitumia vizuri na tunaomba watumie vifaa hivi kwa ajili ya usajili na utoaji wa vyeti kwa watoto.Alisisitiza Kinabo

Aliongeza kuwa utoaji wa vifaa hivyo ni moja ya programu za kampuni hiyo kusaidia na kushirikiana na serikali kwenye sekta mbalimbali kwa ajili ya kusaidia watoto ambao hawajapata usajili ili kuweza kupunguza gharama na usumbufu kwa wazazi ili kuhakikisha watoto wao wanapata vyeti hivyo.

Naibu waziri wa wizara ya katiba na sheria Geoffrey Mizengo Pinda akizindua vifaa vya uendeshaji wa zoezi hilo,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Jerry Muro akimuwakilisha Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddy Kimata pamoja na mwakilishi kutoka RITA.
Naibu waziri wa wizara ya katiba na sheria Geoffrey Mizengo Pinda akikabidhi vifaa hivyo kwa Naibu katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia masuala ya afya Dkt.Sifuni Mchome katikati ni Arusha,Mkurugenzi wa kampuni ya mtandao wa simu Tigo Tanzania,Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo wakiwa katika uzinduzi huo
Naibu waziri wa wizara ya katiba na sheria Geoffrey Mizengo Pinda akigawa cheti cha kuzaliwa ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa mpango wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Arusha na Manyara uliofanyika jijini Arusha,katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ndg.Joseph Joseph Mkirikiti
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...