KAMPUNI ya simu TECNO kupitia toleo lake jipya la TECNO Camon 17pro kupita Mkoa kila mkoa (Road Show) kwa lengo la kutaka kila Mtanzania ashuhudia majaabu ya MP48 ya simu ya TECNO Camon 17PRO. TECNO Camon 17pro ni simu yenye teknolojia ya hali ya juu hasa upande wa camera mbele ikiwa na MP48 na 4K video resolution na nyuma ikiwa na MP64.

Zoezi hilo la kutembelea Mkoa kila Mkoa limeanza rasmi jijini Dar es Salaam na wadau wengi wa simu za Mkononi wameonekana kufurahishwa na mbinu waliyoitumia TECNO kuwafikia wateja wake.
Alisikika mdau mmoja akisema, “TECNO wamenipa hamasa ya kununua simu hii ni simu nzuri na camera ndio usiseme sitaki kuikosa TECNO Camon 17pro tena kwa kipindi cha sikukuu thubutu lazima nijipatie yangu mapema sana.”

Hakika tuwapongeze TECNO ni jambo jema sana kutufikia wateja wao mana sio wote tunapata muda wa kwenda madukani lakini kinachofurahisha zaidi ni jinsi hii simu ilivyonyepesi nashukuru nmepata uzoefu mzuri wa kuifahamu kitaaluma zaidi mana huwa tunasikia processor ila mtu haufahamu ni nini ila leo ndio nmepata kujua umuhimu wa processor, memory na mengineyo, alimaliza.

TECNO Camon 17pro ina GB128+8Ram lakini pia ina G90 processor kwa pamoja vinaifanya TECNO CAMON 17pro kuwa simu yenye uwezo wakuhifadhi na kufungua applications au files zenye ujazo mkubwa pasipo kupata joto.
 TECNO inawataka wapenzi wa simu za mkononi kukaa tayari kupata elimu kuhusu kila sifa ya TECNO Camon 17pro. TECNO imejipanga kulifanya hili kwa kutembelea Mikoa zaidi ya mitano nchini Tanzania lakini pia Afisa Mahusiano TECNO, Bwana William Motta ametutakia watanzania wote kheri ya maandalizi ya sikuku ya eid lakini pia ametutaka watanzania wote kutembelea maduka ya simu TECNO kwani kuna zawadi nyingi sana kwajili yetu. 

Road show kuenda kupita zaidi ya Mikoa mitano na zawadi nyingi zitatolewa kwa watu wote watakaopata nafasi ya kufika eneo la tukio hivyo basi wa kazi wa Mkoa wa Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya kaeni tayari kumpokea mkali wa selfie. 
www.tecno-mobile.com Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...