Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MRAKIBU Mwandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Pius Lutumo amewakumbusha waendesha bodaboda wanaosafirisha abiria katikati ya Jiji hilo kuhakikisha wanazingatia sheria na kujiepusha na vitendo vya uhalifu.

Akizungumza jana Mei 6,2021,Lutumo amesema wameamua kukutana na waendesha bobaboda hao kwamba ni muhimu kuzingatia sheria ili kujiepusha na ajali wao pamoja na abiria wao.

"Tumeamua kukutana na waendesha bodaboda walioko hapa katikati ya Dar es Salaam , bodaboda wengi wamekuwa wavunjifu wa sheria lakini tulichokiona wanavunja sheria sio kwasababu hawazifahamu bali ni kwa makusudi.Tumeona ni vema tuwambie faida za kutovunja sheria,"amesema Lutumo.

Amefafanua katika kuwakumbusha huko, wamezungumzia baadhi ya makosa na hasa makosa hatarishi yakiwemo ya kutovaa kofia ni kuhatarisha maisha yake na mtu mwingine.Makosa ya kubeba abiria zaidi ya mmoja (mishikaki) nayo ni makosa hatarishi.

"Kupita taa nyekundu au njano ni hatari na kwa kufanya vile anaweza kusababisha ajali , lakini wenzetu waendesha bodaboda wamekuwa si watiifu kwa kupita kwenye Zebra wakati magari yamesimama kwani hiyo imekuwa ikisababisha ajali ya kugonga,"amesema.

Hivyo amesema kupitia kikao cha mafunzo ambacho kimefanyika leo kati ya baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi na waendesha bodaboda wamekumbusha umuhimu wa kutii sheria za barabarani."Pamoja na yote hayo sasa, hawa ambao tumekutana nao hapa na tukakumbusha kuhusu kuzingatia sheria.

"Wao wawe wajumbe kwa wengine ili elimu iwe endelevu.Aidha tumezungumza kuhusu tabia ya baadhi ya waendesha bodaboda kujihusisha na vitendo vya uhalifu.Tunafahamu maeneo ya Posta na katikati ya mji watu wengi wanaopita huko ni wastaaru na wapole.

"Hivyo wakiona matukio haya yanafanywa na baadhi ya watu wa bodaboda wanashanhangaa.Matukio hayo yanaweza kusababisha siku moja kukawa na katazo la pikipiki kutoingia mjini, hivyo ili kusiwe na katazo tumeona ni vema tukakumbushana kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu lakini yote haya yanatokana na maelekezo ambayo tumepewa tuwaambie haya kwani yanaonekana kwenye jamii,"amesema.

Pamoja na kukumbushana huko, waendesha bodaboda hao walipata nafasi ya kuuliza maswali na kutaka ufafanuzi wa masuala kadhaa yanayohusu sheria za barabarani ambapo walijibiwa na kupewa ufafanuzi ambao kila mmoja ulimuwezesha kuelewa na kuridhika.

Alipoulizwa ni jinsi gani jeshi hilo linaweza kutunza siri za watoa taarifa, Mrakibu huyo Mwanamizi amesema Jeshi la Polisi lina weledi mkubwa wa kupokea taarifa na kuzitunza huku akishauri watoa taarifa kupeleka taarifa zao kwenye watu sahihi.

Kwa upande wao waendesha bodaboda hao wamefurahishwa na mafunzo hayo ya kukumbusha kuzingatia sheri yaliyofanywa na maofisa hao wa jeshi la polisi na kwamba wanaomba yawe endelevu.



Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) wa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Pius Lutumo akizungumza na waendasha bodaboda wanaofanya safari zao katikati ya Jiji hilo kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria na kujiepusha na vitendo vya uhalifu.

Waendesha bodaboda wanaotoa huduma ya kusafirisha abiria kati kati ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye kikao cha kukumbushwa kuzingatia sheria wanapokuwa barabarani.

Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) wa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Pius Lutumo akisikiliza swali la mmoja ya waendesha bodaboda wanaosafirisha abiria katikati ya Jiji hilo.
Pius Lutumo ambaye ni Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) wa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na waendesha bodaboda wanaobeba abiria katikati ya Jiji hilo.

Mmoja ya waendesha bodaboda wanaotoa huduma ya kusafirisha abiria katikati ya Jiji la Dar es Salaam akiuliza swali kwa Pius Lutumo ambaye ni Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) wa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

Waendesha bodaboda wa katikati ya Jiji la Dar es Salaam wakimsikiliza mwenzao alipokuwa akitoa ushauri wakati wa kikao hicho. Pius Lutumo ambaye ni Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) wa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao kati yake na waendesha bodaboda wanaotoa huduma ya kusafirisha abiria katikati ya Jiji hilo.


Mmoja ya viongozi wa waendesha bodaboda Abdallah Bakari akisisitiza jambo wakati wa kikao kati yao na maofisa wa Jeshi la Polisi waliokuwa wakikumbusha umuhimu wa waendesha bodaboda kuzingatia sheria na kujiuepusha na vitendo vya uhalifu.


Waendesha bodaboda wanaosafirisha abiria katikati ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Mrakibu Mwandamizi wa jeshi hilo kutoka Kituo cha Polisi Kati Pius Lutumo baada ya kikao cha kukumbusha uzingatiwaji wa sheria barabarani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...