Na.Vero Ignatus,Arusha

Wafanyabiashara wametakiwa kujenga tabia ya usafi katika maeneo yao ya biashara, ili kuepukana na magonjwa ya mlipukao kama vile kipindupindu na mengineyo,kwani usafi ni afya kinga

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.John Pima mara baada ya kushiriki katika usafi wa mazingira katika soko kuu ,ambapo amewataka kutambua kuwa wajibu wa usafi ni wa kila mmoja mwenye kibanda au vizimba eneo la soko,hivyo watambue maisha na usalama wawatu, hauwezi kuachwa kwenye watu mwenye nia ovu wanaoacha uchafu unazagaa.

Akizungumza mwenyekiti wa wamachinga jiji la Arusha Amina Njoka amewataka wafanya biashara hao kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni za afya za kutunza mazingira yao ya kazi, bila kukiuka taratibu na kanuni zilizopo ili kuepuka kupata magonjwa ya mlipuko,Pamoja na kuboresha maeneo yao ili watu wavutiwe na bidhaa zao kwani uchafu ni laana moja wapo ya mazingira

‘’Kuna baadhi ya watu wanafanya vituko vya kuchonganisha serikali na wananchi sisi hatupo tayari,wengine wanaweka siasa kwenye mambo ya msingi tunaomba tuondoleeni siasa huu ni mudawa kazi muda wa kujijenga’’ alisema Amina

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha Kenani Kihongosi alimwagiza mkurugenzi wa jiji la Arusha kushirikiana na mkuu wa soko ili kuhakikisha anachukua hatua kwa wafanyabiashara wote wenye vibanda ndani ya soko hawatoki kufanya biashara nje ya soko.

‘’Mkurugenzi kasimamie utaratibu huu,wewe tekeleza kama mtu hawezi kuwa na kibanda ndani, akaacha kisha akaja nje huo ndio utaratibu ,niwaombeni wale wote waliopewa vibanda ndani na mkavitoa nje fanyeni utaratibu wa kuvirudisha ndani haraka iwezekanavyo kwa hiayari yenu tu wenyewe, kwasababu ni ustaarabu tu wa kawaida’’alisema Kihongosi

Aidha mkuu huyo wa wilaya akiwataka wafanyabiashara hao kusimamia usafi wa mazingira katika maeneo yao, kwani mazingira yasipokuwa na usafi kutasababisha mlipuko wa magonjwa mbalimbali,hivyo amewataka kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie

‘’Lazima tuzingatie usafi kwani humu ndipo tunaponunua vyakula tunavyotumia majumbani mwetu,yaani niwaambie uchafu ukiendelea tutachukua hatua stahiki ambazo sisi hatupendi tugombane na wananchi tunatamabi wananchi wafanye biashara kwa uhuru mkubwa sana lakini tuzingatie usafi’’alisema Kihongosi

Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara katika soko kuu Jijini Arusha ndugu Fred Mollel ,aliushukuru uongozi wa jiji na wilaya kutembelea soko hilo na kuona changamoto wanazozipitia

‘’Wakati ule nachaguliwa kuwa mfanyabiashara wa soko tayari nilishakuta wafanyabiashara wametoka nje ya soko ,tumekuwa tukishiriki vikao mbalimbali lakini bado ilikuwa ngumu maana lilikuwa ni agizo,hivyo tunaomba serikali ijaribu upya suala hili’’ alisema Mollel

kwa upande wake mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Chudaa Hassani alitoa dukuduku lake kwa niaba ya wamachinga wenzie ,mbele ya mkurugenzi na mbele ya mkuu wa wilaya juu ya namna ambavyo wafanyabiashara wenye vizimba na vibanda ndani na kuvitoa nje ya soko na kuwa kero kwa wengine hivyo kuwaomba wawatatulie changamoto hiyo .

‘’Mkuu ukiangalia kuanzia meza ya kwanza hadi ya mwisho kwenye barabara hakuna gari zinazopishana hapa,hakuna maegesho ya magari ya biashara,hatuna mahali pa kukupata mkurugenzi na mkuu wa wilaya leo tutatulie changamoto hii’’Alisema Chudaa. 

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt John Pima akizungumza na wafanyabiadhara na wa soko kuu Pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali wanazozipitia.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenani Kihongosi akizungumza na wafanyabiadhara na wa soko kuu Pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali wabazozipitia.

Bi Amina Njoka mwenyekiti wa wamachinga katika Soko kuu akiwasisitiza wafanyabiadhara hao kufuata utaratibu uliowekwa ili kutokuvunja Sheria .

Mkuu wa soko ndugu Fred Mollel akijibu maswali baada ya wafanyabiashara katika Soko kuu kuvuruga utaratibu wa kutoka nje kufanya biashara na kuacha vizimba vyao ndani ya Soko.

Bi Chudaa Hassan mfanyabiashara akitoa dukuduku lake mbele ya Viongozi walipofika sokoni hapo kufanya usafi wa mazingira na kuelezea changamoto wanazozipitia baada ya utaratibu kuvurugwa.

Wafanyabiadhara katika soko kuu Jijini Arusha wakiwasikiliza Mkurugenzi wa Jiji Dkt.John Pima pamoja na mkuu wa wilaya hiyo Kenani Kihongosi Mara baada ya kushirikiana nao katika usafi wa mazingira katika soko hilo.

Arusha Jigging Club wakiwa katika eneo la soko kuu tayari kwa kufanya usafi wa mazingira.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenani Kihongosi akishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira katika soko kuu Jijini Arusha.

Baadhi ya wafanyabiadhara na wadau katika Soko kuu jiiini Arusha wakiwasililiza Viongozi Mara baada ya kushirikiana kufanya usafi wa mazingira katika Soko hilo.

Pichani ni wafanyabiashara katika soko kuu Jijini Arusha wakishangilia Mara baada ya tamko kutoka kwa Mkurugenzi kwamba wafanyabiashara waliotoa vizimba ndani na kuweka nje ya soko warudi ndani ya soko kuendelea na biashara.

Wafanyabiadhara katika soko kuu Jijini Arusha wakimsikiliza Mkurugenzi Dkt.John Pima mara baada ya kushiriki zoezi la usafi wa mazingira katika soko hilo.

Usafi ukiendelea katika Soko kuu la Jijini Arusha

Baadhi ya Wana Arusha Jogging wakuendelea na usafi Kama wanavyoonekana katika Picha

Wafanyabishara wa soko kuu wakufuatilie kile kibachozungunzwa na Mkurugenzi Dkt.John PimaMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...