·        Ni kuhusu mfumo wa ununuzi wa mazao kupitia Ushirika

·        Washangaa wabunge Hasunga, Njalu, kutetea walanguzi

 

Na Woinde Shizza, Michuzi Tv Arusha

SIKU chache baada ya Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, kutoa ufafanuzi Bungeni kuhusu umuhimu wa mfumo wa ushirika katika ununuzi mazao ya wakulima na kusisitiza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa Ilani na Sera ya CCM, wakulima wengi wamejitokeza kumpongeza.

 

Mbali na kusisitiza kuwa mfumo huo ndio njia thabiti ya kumlinda mkulima dhidi ya ulanguzi na walanguzi wa mazao vijijini, lakini pia Bashe aliweka bayana kuwa ushirika ni sauti halisi na ya pamoja ya watu wanyonge, kupata masoko ya uhakika na bei nzuri.

 

Naibu Waziri huyo alikuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Vwawa Japhet Hasunga, wa jimbo la Songwe, aliyetaka kujua kwa nini serikali haitaki kuwaachia wafanyabiashara kwenda kwa wakulima vijijini kununua mazao hayo.

 

Mbunge Hasunga, ambaye alikuwa Waziri wa Kilimo katika muhura wa kwanza wa serikali yaawamu ya  tano uliomalizika Oktoba mwaka jana, alionyesha kuupinga mfumo wa ushirika, akisema unawabana wakulima kupata bei nzri ya mazao yao sokoni.

 

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima na wadau wa ushirika, walieleza kushangazwa kwao kutokana na msimamo wa Mbunge Hasunga, kuhusu suala hilo.

 

“Kwa kweli majibu ya Naibu Wazziri Bashe, kuhusu ushirika yalitufanya kufurahi sana, lakini tumeshangaa huyu Hasunga, kumbe ni yeye alikuwa akikwamisha ushirika akiwa Waziri, maana haikuwa rahisi kuuuliza jambo hilo.” Alisema Marko Konzwe, mkulima wilayani Babati.

 

Konzwe, aliongeza kusema mbunge kama Hasunga, anapaswa kujadiliwa ndani ya CCM kwa kuonyesha kupinbgana na ilani ya chama chakr, lakini pia akiwa kama kiongozi aliyesimamia ushirika, hawrzi kuonyesha usaliti wa Dhahiri.

 

Wakulima wengine, wa Longido na Katesh, walilalamikia kauli za wabunge Hasunga na Mbunge wa Jimbo la Itilima,mkoani Simiyu, Njalu Daudi Silanga pamoja na Ahmed Salum, wa jimbo la Solwa, mkoani Shinyanga.

 

“Tunadhani kuna umuhimu wa kuchukua hatua huko kwenye chama, ikiwa kuna wakati wa kutafakari utekelezaji wa ilani na sera za CCM kwa wananchi na hususan wakulima.” Ande Mweta.

 

Wakulima wa Ufuta katika wilaya ya Songwe na Momba, mkoani Songwe, walimpongeza Bashe kwa majibu na msimamo huo wa serikali, wakionyssha kushangazwa na maelezo yaliyotolewa na Hasunga kuhusu ushirika.

 

“Mkuu wetu wa mkoa Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela, amekuwa na jukumu kubwa la kuhamasisha wananchi kuhusu ushirika, lakini alikuwa akikatishwa tamaa na Mbunge Hasunga, wakati akiwa Waziri wa Kilimo, kwani aliwahi kuzuia shughuli za mfumo huo kufanya kazi katika mkoa huo.” Alisema Mwakanosya Ignus.

 

Mwakanosya alkisema wakulima wanadhani, inatakiwa kauli kutoka kwa Waziri Mkuu, kuruhusu mfumo huo ambao ni wa kisera na kiilani, kufanyakazi nchini kote kwani umesaidia wakulima kujikwamua na ulanguzi wa mazao.

 

Wakulima wa Choroko katika wilaya za Bariadi, Maswa,Itilima na Meatu, mkoani Simiyu, pamoja na Kwimba mkoa wa Mwanza walishauri kauli zinazotolewa na viongozi kutosigana na maelekezo ya ilani na kisera kuhusu ushirika.

 

“Huku kwetu RC, DC na Ma DED kila mmoja na msimamo wake, lakini kwenye meza za ofisi zao, wameweka katiba ya CCM, Ilani na Sera, tunawashangaa wanazifanyia kazi gani,mfumo wa ushirika wanaupiga vita na sasa wanatetea walanguzi wa mazao.” Alisema Charles Masunga, mkulima wa Bariadi.

 

Wakulima wa Dengu, katika wilaya za Shinyanga Vijijini, Misungwi, Kwimba na Magu, mkoa wa Mwanza, walilalamikia kukosekana kwa msimamo wa pamoja unaolinda wakulima sokoni, huku wakihoji walanguzi wanapata wapi vibali vya kwenda kufuata mazao ya wakulima vijijini.

 

“Mkoa wa Singida, tunahusika na kilimo cha Alizeti, lakini pia ufuta, kilimo ambacho wananchi hukitegemea kukuza uchumina kusomesha watoto, wetu, lakini shida kubwa ni ulanguzi unaoonekana kushamiri kwa kasi na hasa wilaya ya Manyoni, maana hata geti kuu la KINTIKU linahujumiwa na wakubwa.” Alisema Nathanie Limamu.

 

Alisema wananchi wengi wamepata faraka kusikia kauli ya Bashe, kwamba ushirika ni suala la kisera, hivyo wanahitaji kushiriki kikamilifu kuimarisha mfumo huo unaotumika hivi sasa kuuza na kununua mazao ya wakulima kupitia vyombo vya serikali.

 

Waliongeza kusema, Bunge ni chombo kikubwa cha Kitaifa kinachoweka mijadala yake kwa maslahi ya wananchi, haiwezekani kuona mtu anatumia nafasi ya uwepo wake ndani ya chombo hicho kuwahujumu wakulima na kutetea walanguzi wa mazao.

 

“Mfumo wa ushirika, umekuwa na changamoto kadhaa, lakini vema kufanya maboresho ili kuufanya ufanye kazi kwa ufanisi, umekuwa na faida kubwa kuliklo hasara kwa wakulima, ushirika ni sauti ya wakulima kama alivyosema Naibu Waziri Bashe.” Alisema Mweta.

 

Hata hivyo, aliishauri serikali kuangalia utendaji wa bodi zake mbili ile ya Nafaka na Mazao mchanganyiko (CBP) na Stakabadhi za Ghala (WRRB) , kutokana na mazingira ya urasimu unaosababisha walanguzi kuziona kama lango.

 

“Bodi zenyewe haziko kwa ajili ya kuangalia changamoto za wakulima, badala yake zimejenga urasimu kukabiliana na wadau wanaounga mkono ushirika na kuwawekea vikwazo vya kjusajili maghala yao, lakini wanaruhusu maghala ya walanguzi wa mazao.” 

 

Kulingana na wananchi hao, kauli ya Bashe bungeni, imewasaidia wakulima wengi kuelewa maazimio ya kuwepo kwa mfumo huo sio jambo la hiari bali ni matakwa ya Ilani na sera ya CCM, na kwamba kupingana nao ni usaliti wa wazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...