Na.Samwel Mtuwa - Geita.

Waziri wa Madini Doto Biteko  amewataka wachimbaji wadogo wa madini mkoani Geita kutumia taarifa za kitaalam za jiosayansi pamoja na kuitumia Maabara ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) katika shughuli zao za uchimbaji Madini nchini.

Biteko amesema hayo wakati wa ufunguzi WA mafunzo kwa wachimbaji wadogo yanayohusu Namna Bora ya Uchukuaji wa Sampuli za Uchunguzi na Uchenjuaji wa Madini Tanzania yanayotolewa na (GST).

Akizungumzia Juu ya maendeleo ya sekta ya Madini nchini , Waziri Biteko alisema kuwa tafiti za jiosayansi zinazofanywa na GST zinapelekea kugunduliwa kwa migodi mbambali nchini ikiwemo migodi ya wachimbaji wadogo.
Sambamba na  hapo Waziri Biteko aliwapongeza wachimbaji Kwa kufikia mchango wa asilimia thelathini (30%) akilinganisha na awali ambapo wachimbaji wadogo walikuwa hawafikii hata asilimia kumi (10%) katika kuchangia pato la Taifa (GDP).

Akiitimisha  hotuba ya kufungua mafunzo hayo Biteko aliwasisitiza wachimbaji wadogo kutumia fursa ya mafunzo hayo ya nadharia na vitendo ili kuleta tija zaidi na kufanya uchimbaji wa uhakika bila kupoteza muda na mitaji pamoja na kuzuia uharibifu wa mazingira.

Mafunzo haya yanatolewa katika mikoa tisa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...