Wadau wa mazingira kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kmaliza kwa warsha iliyokuwa na lengo la kujadili kuhusu taarifa zinazohusu mamlaka ya hali ya hewa pamoja na kuangalia namna ya kuendeleza harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Can Tanzania Dk.Sixbert Mwanga  akizungumza na wadau wa mazingira kutoka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali zaidi ya 30 ambao wako chni ya mwavuli wa Can Tanzania ambao walikutana kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi.
Mmoja wa wadau wa mazingira akitoa maoni yake wakati wa majadliano hayo yaliyofanyika mkoani Dar es Salaam.
Mtalaam wa Rasilimali za Asili na mabadiliko ya tabianchi Abdallah Isaa akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada wakati wa warsha hiyo.
Wadau wa mazingira wakiendelea na majadiliano ili kutoa mtazamo wao wa nini kifanyike katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na masuala mengine yanayohusu taarifa za hali ya hewa.
Mkuu wa Programu Can Tanzania Boniveture Mchomvu akiwa makini kufuatilia mada wakati wa warsha hiyo.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mada wakati warsha hiyo ikiendelea.
Meneja Miradi kutoka Shirika la Pelum Tanzania Rehema Fidelis akichangia mbele ya wadau hao wa mazingira.
Mkurugenzi Mkuu wa Can Tanzania Dk.Sixbert Mwanga akisisitiza jambo.





Matukio mbalimbali katika picha wakati warsha hiyo ya wadau wa mazingira ikiendelea (PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE.)


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WADAU wa mazingira kutoka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali zaidi ya 30 likiwemo Shirika la Can Tanzania wamekutana mkoani Dar es Salaam kujadiliana kwa kina kuhusu kujadiliana kwa kina na kuona jinsi gani wanachagiza au kuongeza mchango wa taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania.

Wamesema wamechambua kwa kina hasa tafiti  zinazofanywa kwenye masuala ya taarifa zenyewe na ushauri unatolewa na mamlaka hiyo ili sasa wananchi waweze kuhuhisha shughuli zao za kila leo, lakini pia kuhakikisha jamii inapunguza atahari zinatokana na mabadiliko ya TabiaNchi

Kwenye shughuli za kilimo, ufuguji, uvuvi na usafirishaji na sekta nyingine, aidha wamejadiliana kuhusu mchango wa nishati jadidifu katika kuchagiza maendeleo endelevu nchini na hiyo ni pamoja na kuhakikisha nishati hiyo inauhuishwa katika sekta za uzalishaji

Akizngumzia kuhusu warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Can Tanzania Dk.Sixbert Mwanga amesema mbali ya majadiliano hayo wametengeneza kamati kamati mbili , moja itakuwa inafanya kazi na Mamlaka ya hali hewa ili kusaidia hizo taarifa zinawafikia walengwa.

Pia kwa upande wa nishati kusaidia na Serikali hasa Wizara ya Nishati yenyewe ili kuhakikisha mchango wa nishati jadidifu unaongeza uzalishaji na kuchangia ukuaji wa uchumi wa pamoja.

Amefafanua licha ya jitihada zinazoendelea kwa watu wa kawaida bado wengi hawajambua mchango unaotolewa a mamlaka ya hali hewa ukizingatia wakulima wanajilimia tu kwani wanajua mvua zinanyesha Oktoba.

"Mkulima haanzi kuuliza kwa Mamlaka ya hali ya hewa kuwa inasema nini, kwa hiyo analima na kisha anapanda mazao hajui kama mvua zitanyesha kwa kiwango gani.Kama mfugaji afuge kuelekea wapi?Kama msimu mzima kutakuwa hakuna mvua basi apunguze mifugo yake.

"Kwa maana ya malisho yatakuwa hayapo, hivyo hivyo kwa wavuvi kuangalia ni lini aende baharini maana kunaweza kuwa na upepo mkali , hasa kwa nyakati hizi ambazo athari za mabadiliko ya tabianchi yanazidi kuongezeka , tunaingia baharini upepo mkali watu wanazama,"amesema.

Dk.Sixbert amesema kwa upande wa nishati jadidifu kama Taifa tafiti zinaonesha nchi inakiwango kikubwa cha nishati jadidifu na chenye ubora wa hali ya juu, kwa mfano kuzalisha kwa kutumia upepo na kuzalisha kwa kutumia jua.

"Mchango wa sekta ya nishati bado mdogo, Taifa linakadiriwa linatumia asilimia tatu tu mpaka nne ya nishati jadidifu iliyopo nchini wakati tunalo jua la kutosha, tuna upepo mwingi, kuna mawimbi ya baharini.Hatufanyi uwekezaji wa kutosha kwenye nishati jadidifu.

"Kwa hiyo  hali sio nzuri na tunadhani ni vema tungeweza kuwekeza hata asilimia 50 kwa 50 ukilinganisha na mataifa mengine ambayo yapo yamefikia asilimia 10, 20 hadi asilimia 30 na kuendelea katika matumizi ya nishati jadidifu,"amesema.

Ameongeza wangefurahi kuona mchango wa nishati jadidifu unaongezeka katika kupambana na umasikini wa nishati."Auhitaji kupeleka gridi ya taifa kwa  kusimika nguzo kutoka hapa mpaka kule, sehemu ambayo sio lazima kuweka nguzo maana hakuna watumiaji , kule inahitajika kuweka Sola itakayozalisha umeme na wana kijiji wakatumia".

Alipoulizwa nini kifanyike ,Dk.Sixbert amesema lazima kuwepo na sera ya nishati jadidifu.Wizara iwe na sera ya nishati jadidifu badala ya kuwa na sera ya nishati ambayo ina mambo yote yote yanayohusu nishati.

"Kwa hiyo wakiangalia nishati ya wakiona inaendelea hakuna anayeangalia nishati jadidifu kama inaweza kuchagiza maendeleo endelevu.Pili sasa tuanze kutenga fedha za kutosha za kufanya uwekezaji ndani ya sekta ya nishati jadidifu yenyewe na hii inaenda moja kwa moja , kwa mfano ziko fedha za moja kwa moja kwenye mifuko ya mabadiliko ya tabianchi."

Aidha amesema yanaweza kufanyika mazungumzo kati ya nchi na nchi au nchi na mabenki ili kuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha wanakwamua mkwamo ulioko kwenye matumizi ya sekta ya nishati jadidifu.

Pia amesema  kuna haja ya kuwa na mkakati wa kuangalia ubora wa sola ambazo zinaingia nchini kwani kuna malalamiko ya baadhi ya sola kuwa na kiwango kilichokuwa chini ya ubora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...