Na PATRICIA KIMELEMETA.


MAADHIMISHO ya uchangiaji wa damu yanafanyika kila mwaka Duniani kote ambapo Shirika la Afya Duniani(WHO) limewahamasisha wadau mbalimbali wanajitokeza kaa ajili ya kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa mbalimbali wakiwamo mama mjamzito na watoto chini ya miaka mitano.

Maadhimisho hayo ambayo yanafanyika Juni 14, Duniani kote,WHO imekua ikihamasisha wadau kuona umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wakiwamo wajamzito na watoto chini ya miaka mitano ambao wanasumbuliwa na maradhi mbalimbali yanayohatarisha maisha yao.

Hivyo basi Upatikanaji wa damu salama ni sehemu ya utekelezaji wa lengo la huduma za afya kwa wote lakini pia ni kipengee muhimu katika utendaji kazi wa mifumo ya afya kote duniani.
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) ni miongoni kwa hospitali zinazohitaji damu kwa wingi kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali hiyo wakiwamo watoto chini ya miaka mitano pamoja na wajawazito.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dk. Plaxeda Ogweyo aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia damu ili iweze kuwasaidia wajawazito na watoto waliolazwa katika hospitali hiyo ambao wana uhitaji wa damu kwa ajili ya matibabu yao.
Amesema kuwa, uhitaji wa damu katika hospitali hiyo ni mkubwa kwa sababu unasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa, wakiwamo wajawazito na watoto ambao wanpatiaa matibabu hospital in I hapo.

"Hospitali ya Muhimbili ina uhitaji mkubwa wa damu, kwa sababu tuna wagonjwa wa aina mbalimbali wakiwamo wajawazito na watoto chini ya miaka mitano, hivyo basi tutaendelea kuhamasisha wadau mbalimbali kujitokeza na kuchangia damu ili iweze kuwasaidia wagonjwa wetu," amesema Dk. Ogweyo.

Amesema kuwa,hospitali hiyo inahitaji chupa 100 hadi 120 kwa siku na kwamba kiwango cha ukusanyaji damu kwa siku ni chupa 70 hadi 100 ambacho ni kidogo na hakikidhi mahitaji kulingana na ukubwa wa hospitali hiyo na mahitaji yake.

Amesema kuwa, hivyo basi mahitaji ya damu bado ni makubwa,kwa ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wataweza kufanikiwa kupunguza ukubwa wa tatizo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...