*N sifa za Infinix NOTE 10 PRO NA SAMSUNG GALAX A51)

Infinix tangu kutambulishwa Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 2018 imekuwa na ushindani mkubwa sana na makampuni mengine ya simu kama Samsung. Infinix na Samsung wamejikuta katika ushindani mkubwa hasa kwenye simu hizi mbili Samsung A51 na Infinix NOTE 10pro.


Kamera
Infinix NOTE 10pro na Samsung A51 zinabaadhi ya sifa za kufanana kama uwepo wa kamera 4 nyuma isipokuwa kamera kuu ya Infinix NOTE 10 pro ni ubora zaidi kulingana na namba ya pixel NOTE 10 pro ikiwa na MP64 na A51 ni MP48 na kwa sababu hii tunasema Infinix imefaulu kwani Kamera ya nyuma ni kamera muhimu sana hasa ukizingatia Kamera ya NOTE 10 pro inauwezo hadi wa kuscan document.

Processor
Kwa upande wa processor Infinix Note 10 Pro inatambulika kama simu bora sana kwa ajili ya kucheza game kwani simu hii inakuja na processor ya MediaTek Helio G95 na Samsung Galax A51 inakuja na Exynos 9611. Helio G95 ni pendwa sana kwa wapenzi wa games na Exynos 9611 kasi yake ipo kwenye matumizi ya application nyenginezo na si kwa games kwa hapa tunaweza sema kila simu imefaulu kwa aina yake kutokana na aina ya watu wanaowalenga. Infinix inalenga zaidi vijana wenye kupenda kwenda na wakati na games ni moja ya starehe yao kubwa na Samsung ni kampuni yenye kulenga watu wa makamo basi hadi hapo kampuni zote mbili zimefaulu.


Ram
Kwa upande wa RAM ni wazi kuwa simu hizi zinalingana zote zikiwa na RAM ya GB 8, hapa lakini kwa upande wa Infinix Note 10 Pro unapata toleo lenye GB 8 za RAM huku kwa Galaxy A51 ukiwa unapata matoleo ya GB 4, 6 na 8


Uhifadhi wa Ndani (Rom)
Kwa upande wa uhifadhi wa ndani au ROM, Infinix Note 10 Pro inaongoza kabla hujabisha ngoja nikupe sababu Infinix Note 10 Pro inakuja uhifadhi wa GB 128 na 256 lakini mbali na hivyo sehemu ya kuweka memory card kwenye Infinix Note 10 Pro imejitenga na hivyo una uwezo wa kuweka laini mbili za simu pamoja na Memory card, Infinix Note 10 Pro ina uwezo wa kuchukua memory card ya Hadi TB 2 tofauti na Galaxy A51 ambayo inaweza kuchukua Memory ya hadi TB 1 lakini pia Galaxy A51 haina nafasi ya kueka memory ni lazma uchague ueke line moja ya simu na sim card ya pili uweke memory kadi na si kueka line mbili za simu na memory card kwa wakati mmoja. Hapa tunasema NOTE 10 pro imefaulu.

Sensor
Kwa upande wa Sensor au sensa simu zote zinakuja na sensa ambazo zinafanana ambazo ni Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass. Tofauti kubwa ambayo ipo kwenye Infinix Note 10 Pro ni pamoja na kuwa na sehemu ya Fingerprint pembeni kwenye sehemu ya kuwasha hii itakupa urahisi wa kufikia sehemu hii hata kwa mkono mmoja tofauti na Galaxy A51 ambayo inayo sehemu ya fingerprint kwenye kioo ambayo ni lazima kushika simu kwa mikono miwili.

Battery
Kwa upande wa battery simu ya Infinix Note 10 Pro inaongoza kwenye upande wa battery kutokana na kuwa na battery kubwa ya 5000 mAh ambayo pia inaweza kujaa chaji kwa haraka kutokana na kuwa simu hii inakuja na teknolojia ya Fast charging ya hadi 33 Wh.

Tofauti na Galaxy A51 simu hii inakuja na battery ya 4000 mAh, ambayo inakuja na teknolojia ya fast charging yenye uwezo wa hadi 25 Wh. na hapa Infinix imefaulu.

Sifa Za Nje Muundo
Tukianza na muundo simu ya Infinix Note 10 Pro ni simu bora kwenye kipengele hichi, hii inatokana na simu hii kuwa na muundo mkubwa kuliko Samsung Galax A51. Infinix NOTE 10pro ina urefu (height) inch 6.80, upana (width) inch 3.08, na kina (depth) inch 0.31.

Galaxy A51 ina inch 6.5 lakini ukiangalia kwenye swala la gharama Infinix NOTE 10 pro inapatikana kwa bei rafiki ukilinganisha na sifa zilizopo kwenye simu hiyo hapa tena Infinix amefaulu kwa asilimia kubwa.

Kioo
Tukija kwenye upande wa kioo, Infinix Note 10 Pro pia inaongoza kwenye kipengele hichi kwa kuwa na kioo kikubwa zaidi, Infinix Note 10 Pro inakuja na kioo cha inch 6.95, tofauti na simu za Galaxy A51 yenyewe inakuja na inch 6.

Mbali na hayo Infinix Note 10 Pro inaongoza kwa resolution ikiwa na resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2460, na Galaxy A51 ikiwa na resolution ya chini huku ikiwa inakuja na resolution ya pixel 1080 kwa 2400.

Upatikanaji
Kama umeelewa vizuri tofauti za hizi simu mbili basi kwa upatikanaji wake tafadhali
tembelea duka lolote la simu karibu yako.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...