MWANAMITINDO na msanii  Hamisa Hassan, maarufu kama hamisa Mobeto ateuliwa kuwa mmoja wa balozi wa kuhamasisha watu juu ya swala zima la ulipaji wa  kodi leo 22 Juni 2021 bungeni jijini dodoma, waliochaguliwa engine ni Edo Kumwembe, Sammata

Waziri wa fedha na mipango Dkt.Lameck Mwigulu Nchemba leo bungeni jijini dodoma amemteua Mwanamitindo Hamisa mobeto kuwa mmoja wa mabalozi wa kuhamasisha watu kuhusu swala zima la ulipaji wa kodi.

 Kupitia ukurasa  instagram Hamisa mobeto ameposti na kuandika kwa kutoa shukurani kwa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na waziri wa fedha na mipango kwa kumuamini na kumteua kuwa balozi wa uhamasishaji wa ulipaji wa kodi. 

Pamoja na kuwa na ubalozi wa kampuni tofauti tofauti kutangaza pedi kupitia HQ pads kutangaza urembo wa nywele za rasta kupitia kampuni ya Prima Afro siku ya leo bungeni Dodoma amepata shavu kubwa kwa kuteuliwa kuwa balozi wa kuhamasisha watu kwenye suala la zima la ulipaji wa kodi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...