Na Mathew Kwembe, Mtwara

Wanariadha mahiri kutoka mikoa ya Kigoma, Mtwara na Ruvuma wametia fora katika fainali za mbio za mita 100 za riadha maalum ambazo zimefanyika leo asubuhi katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Mtwara.

Wanariadha kutoka mikoa hiyo walijizolea medali nyingi kuliko mikoa mingine iliyoshiriki fainali hizo maalum za UMITASHUMTA kwa mwaka huu 2021 ambapo kila mkoa wanariadha wake sita walijishindia medali baada ya kushika mojawapo kati ya nafasi nne za juu kwenye mashindano hayo.

Mikoa iliyofuatia kwa kupata medali nyingi ni Mwanza, Lindi, Mbeya, Njombe, Tabora, Morogoro, Tanga, Pwani na Kilimanjaro baada ya wanariadha watano kutoka kila mkoa huo kujizolea medali maalum.

Wanariadha wanne kutoka mkoa wa Arusha nao walijizolea medali maalum baada ya kushika nafasi nne za juu za fainali hizo.

Mkoa wa Arusha ulifuatiwa na wanariadha kutoka mikoa ya Singida, Iringa na Manyara ambao kila mmoja ulijizolea medali tatu.

Mikoa ya Songwe, Rukwa na Shinyanga kila mmoja ulitoa wanariadha wawili waliopata medali huku mikoa ya Dar es salaam, Dodoma na Geita ikifanikiwa kupata medali moja kwa kila mkoa.

Mbali na mbio za mita 100 fainali maalum pia kulikuwa na mbio za mita 100, wavulana na wasichana hatua makundi, kurusha tufe kwa wavulana na wasichana, mbio za mita 200, mita 1500 na mbio za kupokezana kijiti 4 x mita 100 kwa wavulana na wasichana.

Mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga na Mara ilitia fora katika hatua hii kufuatia wanariadha wake wengi kufanya vizuri katika hatua ya mchujo na hivyo kufanikiwa kusonga mbele.

Mashindano ya riadha yaliyoanza leo yataendelea kufanyika hadi tarehe 18/6/2021 ambapo washindi mbalimbali watajinyakulia medali na vikombe

 

Mwanariadha Sylvester James wa shule ya msingi Mwalwigi kutoka wilaya Misungwi akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kushika nafasi ya pili kwa upande wa wanaume katika mbio za mita 1500 hatua ya mchujo katika michuano ya riadha ya UMITASHUMTA iliyofanyika leo asubuhi viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.

 

 

Mwanariadha Tano Machiya kutoka Tabora (kulia) akiwa mbele ya wanariadha wenzake Baraka Mussa wa Tabora (kushoto), Shigera Shigera wa Shinyanga, Tegemea Simon wa Dodoma (katikati) na Uzaima Juma wa Singida wakimalizia mbio za mita 100 katika fainali zilizofanyika katika uwanja wa chuo cha ualimu Mtwara leo asubuhi.


 Mwanafunzi Masanja Igoko (Kulia) Kutoka Msalala, mkoani Shinyanga akifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika hatua ya mchujo ya makundi katika mbio za mita 1500 zilizofanyika leo mjini Mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...