Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala wakizindua mfumo wa HAKI YANGU App ambao umebuniwa na LSF kwa ajili ya kumsaidia mwananchi kupata huduma ya msaada wa kisheria popote alipo kupitia simu yake.  Tukio la uzinduzi limefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akionyesha jinsi mfumo wa HAKI YANGU App unavyoweza kufanya kazi kupitia simu ya mkononi.  Mfumo huo umebuniwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF) kwa ajili ya kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa mwananchi kupitia simu ya mkononi popote alipo.
Sekretarieti ya Shirika la Legal Services Facility (LSF) ikiwa pamoja Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palagamamba Kabudi (katikati waliokaa) mara baada ya tukio la uzinduzi wa mfumo wa HAKI YANGU, ambao unaweza kumsaidia mwananchi kupata huduma za msaada wa kisheria mahala popote alipo kupitia simu yake ay mkononi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala (kulia) akimkabidhi tuzo ya Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba kwa niaba ya Wizara yake kutokana mchango wa Serikali katika kukuza upatikanaji wa haki kwa wananchi kupitia huduma za msaada wa kisheria.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala akizungumza wakati wa tukio la uzinduzi wa mfumo wa HAKI YANGU App leo jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.

 

SHIRIKA linalotoa Msaada wa kisheria(LSF) nchini limezindua Mfumo wa kitumizi cha simu za mkononi unaojulikana Kama "HAKI YANGU APP" ambao utaweza Kumsaidia mwananchi kupata msaada wa kisheria popote alipo kupitia simu yake ya mkononi.

Akizungumza na Waandishi Wahabari wakati wa Uzinduzi wa Mfumo huo jijini Dar es salaam,Waziri wa katiba na Sheria nchini pro.Palamagamba Kabudi, amesema kuwa Shirika Hilo la (LSF) imekua ni Mdau muhimu wa serikali hasa katika Sekta ya msaada wa kisheria kwa kuwa imekua Mstari wa mbele na kuwezeshwa upatikanaji wa haki kwa wananchi kupitia Mradi wake wa upatikanaji wa haki.

"Shirika linaakotoa msaada wa kisheria (LSF )imekuwa ikichagiza mabadiliko ya kisera na kimfumo katika Sekta ya msaada wa kisheria kwa Kushirikiana kwa karibu na Serikali."

Aidha,Kabudi ameeleza kuwa mwaka 2017 walishirikiana kwa karibu na ( LSF )katika kuhakikisha Sheria ya msaada inatungwa ili kuwezesha wananchi wetu kupata haki zao kupitia huduma za msaada na wasaidizi wa kisheria.

"Nimefurahi kuona Shirika hilo wamekuja na mfumo ambao utasogeza huduma karibu zaidi na wananchi wanaohitaji huduma ya msaada na wasaidizi wa kisheria."

Pia Kabudi amesema Serikali ya awamu ya sita natambua mchango walionao Wadau wa Maendeleo nchini ikiwemo Sekta binafsi pamoja na Sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali katika kuunga Mkono juhudi za Serikali kwenye kuboresha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo huduma ya msaada wa kisheria na upatikanaji wa haki kwa ujumla kwani ni muhimu katika kuchochea Maendeleo ya kijamii na uchumi kwa ujumla.

Kwa upande wake,Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika linalotoa msaada wa kisheria (LSF) Lulu Ng'wanakilala amesema kuwa wamebuni Mfumo wa "HAKI YANGU APP" ili kuendelea kuhakikisha kuwa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria nchini zinapatikana kiurahisi zaidi kwa kuwa upatikanaji huduma hiyo imekuwa changamoto katika jamii licha ya umuhimu wake.

"Kwa uzoefu wa (LSF) katika kutekeleza Mradi wa upatikanaji wa haki nchini tumeona kuwa wananchi walio wengi bado wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hivyo njia hiyo itachochea upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa urahisi na mahali popote kupitia simu ya mkononi."

Hata hivyo Ng'wanakilala ameongeza kuwa takribani miaka 10 wamekua wakiwezesha mashirika yanayotoa huduma za msaada na wasaidizi wa kisheria zaidi ya 200 nchi nzima ili kutoa huduma hiyo atika jamii bure.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...