Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), Masoud Othman Masoud akisalimiana na viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo alipowasili kwenye Hoteli ya Lamada kushiriki Kikao cha Kamati Kuu ya Kawaida kinachofanyaka hotelini hapa leo.

Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), Masoud Othman Masoud akisalimia wna kuzungumza na wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo alipowasili kwenye Hoteli ya Lamada kushiriki Kikao cha Kamati Kuu ya Kawaida kinachofanyaka hotelini hapa leo.
****************************
Na Mwandishi Wetu

MAKAMU wa Kwanza Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), Masoud Othman Masoud ameahidi kufanya kazi kwa kujituma ili kufanikisha malengo ya Chama cha ACT-Wazalendo na nchi.

Makamu huyo alitoa kauli hiyo leo Juni 19/2021 wakati akizungumza kwa mara ya kwanza kama mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo kwenye kikao cha kamati kuu cha kawaida kinachofanyika katika Ukumbi wa Lamada Ilala jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Masoud pia Kaimu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Dorothy Semu aliwatambulisha wajumbe wapya wa Kamati Kuu ambao ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Wawakilishi Hassan Hamad Omar na Khalifa Mohammed Omar Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Amesema nafasi aliyopewa na chama hicho ya kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imemuheshimisha hivyo atahakikisha anaitendea haki ili kuwe na matokeo chanya.

“Tupo wengi ndani ya chama na wengine wazito kuliko mimi lakini mliona mimi ndiye nichukue nafasi baada ya kifo cha Mwalimu na Kiongozi wetu Hayati Maalim Seif Sharif Hamad niseme wazi nitajitahidi kwa kila njia kuhakikisha siwaangushi.

Nakumbuma alikuja Katibu na Makamu Mwenyekiti kuniambia natakiwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais niliwajibu hivi mnajua mimi ni fundi Seremala hivyo fundi Uwashi sitoweza wakanijibu kuwa naweza hivyo kwa maslahi ya chama nilikubali na kazi zinaendelea,” amesisitiza.
Masoud amesema kukubali nafasi hiyo ilikuwa mtihani mzito ila anaamini waliomuana waliona uwezo wake hivyo akasisitiza ushirikiano ndani ya chama na serikali ili kuchochea maendeleo na mshikamano.

Aidha, Masoud amewataka wana ACT kutosista kumrekebisha iwapo wataona anapotoka kwa kuwa hakuna mtu mkamilifu.Makamu wa Rais huyo amesema anashukuru chama chake kumpitisha katika nafasi hiyo ya ujumbe wa kamati kuu kwani atakuwa amekamilisha utekelezaji wa majukumu yake kwa sasa.Masoud amesisitiza mshikamano kwa viongozi na wanachama ili kuchochea maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...