JOSEPH MPANGALA-IRINGA

Mpango wa Kurasimisha Rasilimal na Biashara za Wanyonge MKURABITA Imetoa hati za Ardhi za Kilmila 220 kwa wakulima wa Chai wa Wilaya ya Kilolo ili kuweza kuzitumia kwa lengo la kujiongezea Uchumi kwa kukopa katika taasisi mbalimbali za Kifedha

Wakulima hao ambao walianza kwa kupatiwa Elimu ya Matumizi ya Hati hizo ikiwa ni pamoja na kuondoa migogoro ya Ardhi pamoja na Kujiimarisha Kiuchumi.

Akiongea katika hafla ya ugawaji wa Hati hizo Meneja wa Urasimishaji ardhi Vijijini Antony Temu amesema mpaka sasa wamekwisha Zifikia Halmashauri 54 na Kugawa hati zaidi ya elf 70.

“Mkurabita tumeweza tumeweza kufanya Urasimishaji Nchini kwa maana ya Ardhi ya Vijiji katika Halmashauri 54 ambapo tumeshapima mashamba Laki Moja na NNe na Kutoa Hati zaidi ya elf 74 na 666 na kuwajengea uwezo wananchi na kuwaunganisha na Taasisi za Fedha kwa maana ya Benji zetu za NMB,CRDB na Benki ya Posta”Temu

Vijiji Vitano vya wilayani Kilolo Vimepimia ardhi na Kukabidhiwa Hati Bure kwa wakulima wa Chai ili kuweza kutambua Mipaka yao pamoja na kutumia Hati kuweza kuendeleza Kilimo Hicho.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Philemon Namwinga akimkabidhi Hati ya Ardhi ya Pili Filideli Chelestina mkazi wa Kijiji cha Ilamba katika hafla ya kukabidhi hati 220 kwa vijiji vitano vya Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.


Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini Antony Temu akitoa mafunzo ya Faida zainazopatikana kwa kuataumia Hati za Kimila kabla ya wananchii hao Kukabidhiwa Hati za Kimila 220.


Bi Estinelly Magolosa Mkazi wa Kijiji cha Magome akisoma kwa Makini Hati ya Kimila aliyokabidhiwa na mara baada ya kupimiwa ardhi yake na MKURABITA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...