Naibu waziri wa kilimo, Husein Bashe ameviagiza vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri mikopo inayokopa kutoka kwenye mabenki mbalimbali ili ilete tija kwa wakulima wanachama badala kuitumia mikopo hiyo kwenye shughuli za uendeshaji wa miradi isiyo na tija kwa wanachama hao.

Bashe alitoa agizo hilo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa uliofanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara.

Alibainisha kuwa kwasasa baadhi ya vyama hivyo vinapitia wakati mgumu na kukosa tija kwa wakulima kwa kuwa vimeandamwa na madeni kutoka kwa baadhi ya benki, madeni ambayo kimsingi yametokana na matumizi yasiyo na tija kwa vyama hivyo bila kuwashirikisha wanachama.

“Na hii ndio sababu vyama vya ushirika vimekuwa mzigo kwa wakulima ambao kwa sasa wanalazimika kubeba mzigo wa kulipa madeni ambayo hawajahusika kuyatengeneza. ’’ alisema Bashe ambae pia alitaka vyama hivyo kuanzia mwakani vianze kuwanufaisha wakulima badala ya kuendelea kuwekeza fedha kwenye miradi isiyo na tija.

“Mnajua haiingii akilini kabisa kuona kwamba vyama vya ushirika vinatengeneza mabilioni kupitia makato ya wakulima lakini vinashindwa kuwasaidia pale wanapokuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo hata zile muhimu za kifamilia. Fedha zote zinaenda kulipa madeni ambayo kimsingi yamezalishwa na viongozi wanaoongoza vyama hivi kwa maslahi yao binafsi…naomba hili lifike mwisho sasa.’’ Alisema.

Akizungumzia changamoto ya matumizi mabaya ya mikopo kwenye vyama vya ushirika, Meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Happiness Kizigira alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo, benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kuendesha mafunzo kuhusu namna bora ya kutumia mikopo kabla ya kuwapatia walengwa hatua ambayo imesaidia sana kupunguza tatizo hilo.

“Pamoja na mambo mengine lengo la mikopo yetu huwa kuhakikisha tunamsaidia mlengwa kukuza mtaji wake na kufanya shughuli zake kwa ufanisi na ushindani ili atengeneze faida itakayomuwezesha kurejesha fedha kwetu bila changamoto. Hili kufanikisha hili wateja weteja wetu zikiwemo AMCOS wamekuwa wakipata mafunzo ya namna bora ya kuendesha shughuli zao kutoka kwa wataalam tunaoshirikiana nao…hii imesaidia sana!’’ alitaja.

Benki hiyo mbali na kuwa moja ya wadhamini muhimu wa mkutano huo, ilipata fursa ya kuelezea huduma zake mbalimbali kwa wadau hao ikiwemo huduma ya NBC Shambani inayolenga wadau wote wanaojihusisha na biashara ya Kilimo wakiwemo wasambazaji wa pembejeo za kilimo, wakulima na wasafirishaji wa mazao ya kilimo.

“Lengo hasa la huduma hii ya NBC Shambani ni kuwasaidia wadau wa kilimo kutimiza malengo yao ya biashara ya kilimo ambapo inatoa fursa kwao kuwa na akaunti ya vikundi vya wakulima kama vile AMCOS na vikundi vingine pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja,’’ alisema.

“Akaunti ya NBC Shambani kwa vikundi vya wakulima inawawezesha kuweka fedha bila ada ya uendeshaji wa akaunti huku pia vikundi vikifaidika kwa faida nyingi ikiwemo kutokatwa gharama za uendeshaji wa akaunti kila mwezi, kupata taarifa za akaunti bure sambamba na kutokatwa makato ya kuhamisha fedha wakati wa kulipa wakulima wenye akaunti NBC,’’ alifafanua.

Wakizungumzia huduma za kifedha, baadhi ya wadau wa kilimo walisema huduma hizo ni muhimu kwa kuwa kwasasa taifa linapitia mageuzi ya kilimo biashara ambacho ustawi wake kwa kiasi kikubwa unategemea uwepo wa huduma bora za kibenki zinaenda sambamba na mahitaji wa wadau hao.

“Huduma kama NBC Shambani zinatugusa wadau wote tukiwemo hata sisi wafanyabiashara wa mazao ya kilimo na usindikaji. Hii ni moja ya mfano wa huduma ambazo wadau wa kilimo tunahitaji haswa!,’’ alisema Bw Shakiru Kyetema, Mkurugenzi wa Kampuni ya Shayakye Trading Company inayojihusisha na uuzaji wa kahawa.
Naibu waziri wa kilimo, Husein Bashe (Aliesimama) akizungumza na washiriki Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa ulifanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara. Wanaomsikiliza ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Primus Kimaryo (Kushoto walioketi)
Meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Happiness Kizigira (Aliesimama) akizungumza na washiriki Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa kuhusu huduma za benki hiyo kwa wadau hao.Mkutano huo wa siku mbili ulifanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara.
Meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Happiness Kizigira (katikati akifuatilia mkutano huo).
Meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Happiness Kizigira (Kushoto) akizungumza na mmoja wa wadau wa zao la kahawa Bw Shakiru Kyetema, Mkurugenzi wa Kampuni ya Shayakye Trading Company wakati wa mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa ulifanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma. Benki hiyo ilikuwa moja ya wadhamini muhimu wa mkutano huo.
Baadhi ya wadau wa zao kahawa nchini wakifuatilia moja ya agenda kuhusu ustawi wa zao hilo wakati wa Mkutano Mkuu wa wadau wa Kahawa uliofanyika mwishoni mwa wiki jiji Dodoma ukihudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya zinazolima kahawa, wakulima na taasisi zinazoshughulika na kilimo hicho pamoja na wafanyabiashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...