“Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumiliki pikipiki kupitia mkataba wangu na Bolt. Sasa najivunia kumiliki pikipiki yangu mwenyewe, ndani ya kipindi cha miaka minne (4) kupitia mfumo wa usafiri kwa njia ya mtandao. Kwa kipindi hiki nimefanikiwa kuoa na kwa ninamtunza mke na binti yangu kupitia usafiri huu.

Pia nimeweza kutunza akiba ya kutosha na kununua kiwanja ambapo nina mpango wa kuanza kujenga nyumba yetu.

Kweli mfumo wa usafiri kupitia mtandao unawapatia vijana fursa nzuri ya kujiongezea kipato kizuri, na kupanga vyema muda wa kufanya kazi.

Nimeweza kuwapa fursa za ajira marafiki zangu wengi, ambao nao sasa wanafaidika kwa kufanya kazi na Bolt. Nina mengi ya kushukuru na yote ni kwa sababu ya Bolt”.

Huduma ya usafiri wa Bolt kupitia mtandao ipo kila sehemu na abiria wanapata huduma hii kiurahisi kupitia simu zao za mkononi, wakati wowote na mahali popote wanapohitaji huduma.

Kupitia Bolt, najisikia kuheshimiwa na jamii na nimebarikiwa pia kujua sehemu tofauti za jiji la Dar es Salaam. – Dereva Bolt - Dizaya Damiano Bugeraha (24), Tegeta - Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...