Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango (wapili toka kulia) akionesha mfano wa hundi ya zaidi ya sh Bilioni 21.8 iliyokabidhiwa Serikali ikiwa ni gawio kutoka Benki ya NMB,kutoka kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango kwa Niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea mfano wa Hundi ya Shilingi 21.7 Bilioni sawa na ongezeko la asilimia 43 kwa mwaka 2020 Gawio la Serikali kutoka katika Benki ya NMB leo Juni 18,2021 Jijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akizungumza wakati wa kukabidhi gawio la Shilingi 21.7 Bilioni sawa na ongezeko la asilimia 43 kwa mwaka 2020 Gawio la Serikali kutoka katika Benki ya NMB leo Juni 18,2021 Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiagana na Viongozi Wakuu wa Benki ya NMB muda mfupi baada ya kupokea mfano wa Hundi ya Shilingi 21.7 Bilioni sawa na ongezeko la asilimia 43 kwa mwaka 2020 Gawio la Serikali kutoka katika Benki ya NMB leo Juni 18,2021 Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Viongozi Wakuu wa Benki ya NMB muda mfupi baada ya kupokea mfano wa Hundi ya Shilingi 21.7 Bilioni sawa na ongezeko la asilimia 43 kwa mwaka 2020 Gawio la Serikali kutoka katika Benki ya NMB leo Juni 18,2021 Jijini Dodoma

*************************

Benki ya NMB imetoa gawio la Sh21.8 bilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 43 ya gawio la mwaka jana ambalo lilikuwa Sh15.25 bilioni.


Akipokea mfano wa hundi, Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amesema kiasi hicho kimemridhisha kwa mwaka huu lakini akataka waongeze maarifa zaidi ili kutoa gawio la juu ikiwemo kuwekeza katika nchi majirani.

Dk Mpango alisema kiwango kilichotolewa mwaka jana hakikumfurahisha ndiyo maana akaagiza lazima waongeze juhudi lakini kwa mwaka huu amebarikiwa.Gawio lililotolewa jana ni sehemu ya faida ya Sh206 bilioni ambazo benki hiyo ilipata katika msimu wa kuishia desemba 2020 baada ya kuondoka kodi.

Serikali inapokea gawio hilo kutokana na umiliki wake wa hisa asilimia 31.8 ndani ya benki hiyo ambayo kwa miaka 8 mfululizo imekuwa ikipata tuzo ya benki bora nchini.

“Nimefurahishwa sana na hiki mlichotoa, pamoja na mafanikio haya lakini nataka muongeze ubunifu ili mwaka muwe zaidi ya hapa, hata hivyo nakuagiza Waziri wa Fedha kwamba kiasi hiki kikafanye kazi nzuri kwa wananchi ambayo imekusudiwa,” amesema Dk Mpango.

Kuhusu NMB aliwataka kushirikiana na Taasisi zingine ili wakae na benki Kuu (BoT) kujadili kuhusu riba kubwa ambayo bado inatozwa na mabenki na hivyo kusababisha watu washindwe kukopa.

Aliwataka viongozi wa taasisi ambazo Serikali ina hisa lakini hawatoi gawio kwamba wajitathimini vinginevyo watachunguzwa na watakaokuwa wamekiuka kanuni Serikali itawapeleka Segerea hata kama kumejaa.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya NMB Edwin Mhede alisema tayari fedha hizo zilishawekwa katika akaunti ya msajili wa Hazina na kwamba mwakani watakuwa na kiasi kikubwa zaidi kutokana na mwenendo wavyoona.

Mhede alitaja siri kubwa ya mafanikio ya NMB ni ubunifu na kutljituma kwa watumishi wao katika kuutafuta masoko lakini utoaji bora wa huduma unaowabutia watu kuitumia benki hiyo.

Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna alisema mbali na gawio hilo,lakini wamelipa Serikalini Sh245 bilioni kama kodi za tozo mbalimbali na kutumia asilimia moja ambayo ni zaidi ya Sh2 bilioni kwenye huduma za kijamii.

Bi. Zaipuna alisema benki hiyo imefikia mtaji was Sh1.1 trilioni kutoka Sh660 bilioni kwa mwaka 2015 hivyo ukuaji wake unatia matumaini kwamba itaendelea kuwa ni benki bora yenye kutoa huduma kwa viwango vinavyotakiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...