Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine wa Chama, Serikali na Bunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembea kwenye mfano wa Reli ya Kisasa itakayojengwa kutoka Mwanza hadi Isaka mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341 mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa Jiwe la Msingi jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.

Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli  ya Kisasa SGR ambao utagharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Trilioni 3.1


Baadhi ya mawaziri na viongozi wengine wa taasisi
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli  ya Kisasa SGR ambao utagharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Trilioni 3.1. (PICHA NA IKULU).

Msanii wa Singeli Barobaro akitumbuiza huku viongozi mbalimbali wakimtunza katika Sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR katika eneo la Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Buhongwa mkoani Mwanza wakati akiendelea na ziara yake mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021. 
Wananchi wa Mkuyuni na Butimba wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliposimama eneo hilo kuwasalimu leo tarehe 14 Juni, 2021.

 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...