Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Muhsin Kilonzo (kulia) akimueleza mdau namna uchunguzi wa dawa za kulevya unavyofanyika kupitia maabara baada ya mdau huyo kutembelea banda kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya Dawa za kulevya yaliyoanza leo katika Uwanja wa Nyerere Square, Dodoma. Kilele cha maadhmisho ya Siku ya dawa za Kulevya Duniani ni siku ya Jumamosi tarehe 26 Juni, 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (kushoto) akimueleza  kuhusu uchunguzi wa kimaabara wa dawa za kulevya unavyofanyika kwa kutumia mitambo ya kisasa katika Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati Mkuu wa Mkoa akifungua Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka (kulia), akiongea na Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (kushoto) baada ya kutembelea banda la Mkemia Mkuu wa Serikali wakati akifungua Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Dodoma. Katikati ni Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya.
Mdau akipata huduma katika banda la GCLA.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...