SERIKALI ipo tayari kupokea maoni ya wadau mbalimbali katika kuboresha sekta ya Elimu ili kupata wahitimu wenye ujuzi wa kujiajiri, kuajiriwa na kukidhi mahitaji ya uchumi wa kati na viwanda.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo Mkoani Dar es Salaam katika mkutano wa pamoja uliowakutanisha na wadau elimu na kujadili kwa pamoja namna gani kuboresha mitaala ya elimu kwa ngazi ya awali, msingi na sekondari.

Waziri Ndalichako amesema, Mkutano huo ni matokeo ya maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Serikali ya awamu ya sita Samia Suluhu Hassan na ambayo amekuwa akiyatoa kwa nyakati tofauti kuhusu mapitio ya elimu inayotolewa kuzingatia inajenga ujuzi na stadi za kazi kwa watoto wa kitanzania.

Amesema katika kutekeleza maelekezo ya Rais wamekutana na wadau hao na kupitia mitaala kwa kujikita zaidi katika kutoa maoni yenye kuimarisha mitaala hiyo ambayo italenga kujenga ujuzi na stadi za kazi na mwelekeo chanya kwa watoto wa kitanzania.

Amesema, kupitia mkutano huo maoni yatakayotolewa na wadau hao yatatumiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET,) katika kuboresha mitaala katika ngazi msingi kwa mlengo wa ujuzi, maarifa na misingi madhubuti ya uendelezaji wa elimu nchini.

"Msingi imara wa uboreshaji wa mitaala kwa elimu ya msingi ni nguzo imara katika ngazi za elimu zinazofuata na kuwawezesha wahitimu kumudu mazingira na shughuli za maendeleo zinazowazunguka, na niwaombe maoni tutakayoyatoa yawalenge watoto/wahitimu wa ndoto zetu ambao tunasema wakimaliza darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita hawajui chochote.'' Amesema.

Pia Ndalichako amesema Rais Samia amekuwa akisisitiza kuhusu sekta ya elimu kupitia hotuba zake hasa katika suala la mitaala kwa kuangalia mitaala itakayokuza elimu nchini.

"Niwaombe wadau mliojitokeza leo tujadili suala hili tumuunge mkono Rais wetu katika kutoa mapendekezo na maboresho bora katika mitaala itakayojenga ujuzi, maarifa na kujitegemea kwa wahitimu pamoja na kutumia fursa zinazopatikana nchini kwa kuajiriwa na kujiajiri." Amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba amesema kuwa matarajio ya mkutano huo, ni kupatikana kwa uelewa wa pamoja wa Mitaala iliyopo sasa na kupokea maoni ya Elimu na Mitaala itakayorekebishwa.

“Na imani kuwa tutapata maoni mengi yatakayoboresha Elimu yetu nchini,hivyo tushirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha tunafanikisha ubora wa Elimu” alisema Dkt.Aneth.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Prof. Bernadetha Kilian, amesema taasisi hiyo imejipanga vyema kuhakikisha inaboresha mitaala kuendana na mahitaji ya sasa.

Mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET,) umelenga kukutana na kupokea maoni ya wadau kuhusu mchakato wa kuboresha mitaala ya ngazi ya elimu ya awali, msingi na sekondari, mitaala iliyopo na mwelekeo wa Elimu nchini.
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Mh. Prof.Joyce Ndalichako akizungumza mbele ya Wadau wa Elimu (hawapo pichani) wakati akifungua mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Uboreshaji wa Mitaala ya Elimu kwa shule zote za Awali, Msingi na Sekondari hapa nchini,mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City,mkoani Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza katika mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu uboreshwaji wa mitaala nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo mkoani Dar es Salaam
Sehemu ya Meza kuu ikifurahia jambo .
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Aneth Komba, akizungumza katika mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Uboreshaji wa Mitaala ya Elimu kwa shule zote za Awali, Msingi na Sekondari hapa nchini.
Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Prof. Bernadetha Kilian akizungumza katika mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu uboreshwaji wa mitaala nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo mkoani Dar es Salaam
Sehemu ya Wadau wa Elimu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Mh. Prof.Joyce Ndalichako,Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo pamoja na Wadau wengine wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa ukumbini humo kuhusu mchakato mzima wa kuleta mabadiliko makubwa katika mitaala ya elimu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Aneth Komba, akizungumza katika mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Uboreshaji wa Mitaala ya Elimu kwa shule zote za Awali, Msingi na Sekondari hapa nchini.
Wadau mbalimbali wa elimu nchini wakifuatilia kwa karibu mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu uboreshwaji wa mitaala nchini,mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City mkoani Jijini Dar es Salaam

Wadau mbalimbali wa elimu nchini wakifuatilia kwa karibu mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu uboreshwaji wa mitaala nchini,mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City mkoani Jijini Dar es Salaam

Wadau mbalimbali wa elimu nchini wakifuatilia kwa karibu mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu uboreshwaji wa mitaala nchini,mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City mkoani Jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...