Mbunge wa Mchinga mkoani Lindi, Salma Kikwete amehimiza wanafunzi kusoma masomo ya sanyansi na hisabati akisema ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
 
Alisema mafanikio katika masomo ya sayansi na hisabati ndiyo yakatayotengeneza nguvu kazi nzuri na madhubuti ya kuleta maendeleo ya uhakika.
 
Mama Salma alieleza hayo jana katika hotuba yake iliyosomwa na mbunge mstaafu, Zakia Meghji  wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha sita ya shule ya sekondari ya Academic Archievement Open School (AAOS) ya Dar es Salaam. Shule hiyo ya kimataifa inatumia mfumo Cambridge katika utoaji wa elimu yake.
 
Katika mahafali hayo, mke huyo wa rais mstaafu, Jakaya Kikwete, “masomo ya sayansi ndiyo yanayochochea maendeleo na maisha ya watu, ujenzi wa barabara, umeme, kompyuta yote kazi ya uanasayansi,” alisema.
 
Katika hatua nyingine,  alieleza kufurahishwa na namna shule hiyo ilitilia mkazo masomo ya sayansi na hisabati, akiwataka kuendelea kukaza buti katika kufundisha masomo hayo kwa wanafunzi kwa maslahi Taifa.
 
Meghji aliupongeza uongozi wa shule kwa hatua hiyo, akisema ina miaka miwili lakini imeonyesha mafanikio makubwa, huku akiwataka kutombweta katika utekelezaji wa majukumu yao.
 
“Kitu kitakachoweza kuwarudisha nyumba ni endapo ufundishaji na uendeshaji wa  shule hautakuwa mzuri. Lakini kwa taarifa yenu ilivyo na nilivyotembelea shule sitegemei matatizo hayo kujitokeza,” alisema Mama Salma katika hotuba yake ilisomwa na Meghji.
 
Aliwataka viongozi na wafanyakazi wa AAOS kuwa na ushirikiano na mshikamano katika uendeshaji wa shule hiyo, ili kufikia malengo yao na kwamba hakuna jambo litakaloharibika bali mafanikio.
 
Ofisa  Mtendaji  Mkuu wa  AAOS, Rana Ahmed Saada, shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kujiendesha ikiw ni pamoja  kuchelewesha kwa majibu ya kutambuliwa na kituo chao cha mitihani ya Cambridge na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta).
 
“Tumejitahidi kuandika barua ya kuomba kutambuliwa kama kituo cha mtihani cha Cambridge ili vyeti vya wanafunzi wetu vitambuliwe kitaifa wanapoitimu mitihani yao lakini hatujajibiwa hadi sasa. Lengo letu ni kufungua fursa kwa wanafunzi wa kitanzania na mataifa mengine kusoma vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi,” alisema Rana.
 
Alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2019 kama shule huria, lakini wana mpango wa kuanzisha program za ufundishaji kwa wanafunzi QT pamoja na watahiniwa binafsi.

Wanafunzi wa kiume Sekondari ya Academic Achievement wakiwa wanaimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza mahafali ya kuhitimu kidato cha Sita.

Wanafunzi wa kike Sekondari ya Academic Achievement wakiwa kwenye mahafali ya kuhitimu kidato cha Sita.
Mbunge mstaafu Zakia Meghji akiwa katika mahafali ya shule ya sekondari Academic Achievement akiwa na (kushoto) mkurugenzi wa shule ya Academic Achievement Rana Saada (kulia) ni Mshauri na Msimizi shirika la Maendeleo (WAMA) Johari Kandoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...