SERIKALI za Tanzania na Poland zimeingia makubaliano ya kuimarisha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwenye majiji ya Dodoma na Dar es Salaam kupitia utekelezaji wa ujenzi wa miradi wa majitaka katika Mji wa Serikali , kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kwa Jiji la Dodoma na kupunguza kiwango cha upotevu wa maji kwa Jiji la Dar es Salaam .

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi ( Mb ) amesema makubaliano ya Tanzania na Poland ni hatua muhimu kwa Serikali katika kufikia malengo ya kuimarisha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwenye makao makuu ya nchi Dodoma ambayo kutokana na kasi ya maendeleo na ongezeko la watu kumesababisha mahitaji makubwa ya maji kwa jiji hilo .

Mhandisi Mahundi amesema Serikali imejizatiti kumaliza tatizo la upotevu wa maji katika Jiji la Dar es Salaam ambalo kimsingi ni jiji la biashara ni muhimu maji yanayozalishwa yafike kwa kiwango cha kutosha ili kuchochea shughuli za maendeleo na kuongeza mapato kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam ( DAWASA ) yatakayotumika kufanikisha utekelezaji wa mipango yake .

Aidha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje , anayesimamia ushirikiano wa Kiuchumi na aendeleo Bara la Afrika na Mashariki ya Kati , Mhe . Pawel Jablonski amesema kuwa Poland ipo tayari kutekeleza makubaliano yaliyoafikiwa kwa lengo la kuendeleza Sekta ya Maji Tanzania na kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili .

Ujumbe kutoka nchini Poland uliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje , anayesimamia Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo Bara la Afrika na Mashariki ya Kati , Mhe . Pawel Jablonski , Balozi wa Poland nchini Tanzania , Mhe . Krzysztof Buzalski pamoja na maafisa waandamizi kutoka Serikali ya Poland .

Makubaliano hayo ni matokeo ya majadiliano ya takribani miaka mitatu tangu Serikali hizo zilipokutana kwa lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano kwenye Sekta ya Maji nchini .

Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano ya kushirikiana na Poland katika kuimarisha huduma za majisafi nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Poland, Pawel Jablonsiki akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano ya kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha huduma za majisafi na mazingira.
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi na Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Poland, Pawel Jablonsiki wakisaini makubaliano ya kushirikiana kuimarisha huduma za majisafi ma mazingira.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...